Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2020

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI ( MULTI PURPOSE LIQUID SOAP)

*🛑VIFAA MAMA KTK SABUNI YA MAJI*👇🏻ni hivi ndio vinafanya iitwe  sabuni 👇🏻 *Sulphonic acid* *Sless* *Rangi* *Chumvi.* *Manukato* *👉Sulphonic acid* kazi yake kubwa ni kuondoa uchafu wa mahali wakati unatumia sabuni, pia inaongeza uzito na povu ktk sabuni yetu, sulphonic acid ikizidishwa ktk sabuni huleta mchubuko wa mikono kea mtumiaji. *👉Manukato-* kwaajili ya harufu. *👉Sless( ungarol)* Kai yake ni kuleta povu, kuongeza uzito, na pia huondoa uchafu wa mahali wakati unapotumia sabuni. *👉Rangi* Kuleta rangi ya sabuni pekee. *👉Chumvi* Huongeza uzito ktk sabuni, hutunza sabuni isiharibike, pia ikizidishwa hukata sabuni na kuifanya iwe nyepesi Kama maji na kuisha povu. *🛑Hivi ndio👆🏽 vifaa mama ktk utengenezaji was sabuni ya maji* *🛑Vifaa vya nyongeza👇🏻* *📚 Gryselin-* kazi yake kubwa ni kulainisha sabuni na kuzuia michubuko ya ngozi kwa mtumiaji wa sabuni hiyo. *📚 Formaline-* kazi ya yake kutunza sabuni isiharibike, ila formaline ktk

FANYA MAMBO HAYA UKITAKA KUFANIKIWA KTK MAISHA

*🔨🔨NONDO YA WIKI*🔨🔨🔨🔨🔨🔨 Hallow mambo vipi? Ni matumaini yangu kuwa u mzi 1. *NIA THABITI*- Kwanza kabisa inatakiwa uwe na nia thabiti ambayo itakuwezesha kutumia njia mbali mbali ili kufikia malengo yako. Kama waswahili wasemavyo "penye nia pana njia" hivyo ukitaka kufanya kitu hakikisha una nia kweli kweli ili usifanye kwa kujaribu jaribu 2. *JIAMINI UNAWEZA*- Pili amini kwamba ww unaweza na ww ndo mshindi hivyo ukitaka kufanya kitu muhimu zaidi na sema kwamba mimi naweza hiki. Usiangalie watu wengine kwamba mbona flani alifeli kufanya hiki basi na mimi ntafeli no ur wrong jiamini na jione kwamba ww ndo bora zaidi kufanikisha project. Tazama toka ulipozaliwa hadi leo ngazi ngapi umevuka hadi kufika leo hiyo inaonesha kuwa ni mshindi kwa kila ulifanyalo hivyo jiamini ukiamua kufanya kitu unaweza kabisa. Walioweza wana nini na ww ushindwe kwa nini na  ili iwaje yani? *Go* *Go* unaweza usisite 3 *Fanya kitu kilicho ndani ya uwezo wako*- pia jaribu kufanya kitu k

UMUHIMU WA KUTIMIZA NDOTO YAKO

 *Kwanini ni muhimu kutimiza ndoto yako* _Kama hujui kwanini unapaswa kutimiza ndoto yako huwezi kufikia ndoto yako. Sababu ndiyo itakusukuma kupambana na kuhakikisha unafikia ndoto yako_ ~ Wewe unayo sababu? 1. *Ndoto Yako Ndio Urithi Mkubwa Wa Kizazi Chako* _“Utakapokufa na kuiacha familia yako hutaweza kuiachia familia yako kazi yako ya kuajiriwa au mshahara mkubwa unaolipwa sasa”._ ~Joas Yunus 👆👆Kuna uwezekano mkubwa usipoanza kujipanga leo kuiachia familia yako urithi wa ndoto utakayokuwa umetimiza familia yako inaweza kuishi maisha magumu baada ya wewe kutoweka hapa duniani . Kama ndivyo kuna haja ya kupambana kwa hali na mali utimize ndoto yako ili familia yako ije irithi vitu ulivyoviacha wewe. Ni bahati mbaya sana watu wengi wanajifikiria wenyewe ndiyo maana mtu akishapata kazi anaridhika na kazi yake na kusahau kuwa nyuma yake kipo kizazi chake kinachomtegemea yeye atengeneze njia .Je, unataka mwanao akimaliza chuo akaombe kazi wapi wakati una uwezo wa kuanza

JINSI YA KUISHI NDOTO ZAKO

*JINSI YA KUISHI NDOTO ZAKO* 1) MAHUSIANO (Relationships) Wakati tunaendelea na somo hili, naomba kila mtu atulie, akae chini, afumbe macho, atafakari ni kwa namna ipi mahusiano yake na watu wake wa karibu yamechangia yeye kufika hapa alipo, inawezekana ni pazuri ama pabaya kulingana na kila mmoja wetu ana ndoto tofauti na mwingine. Tafakari kwa kina kisha mwishoni nitakupa nini cha kufanya kusimamia mahusiano yako ili yawe daraja katika kuziishi ndoto zako. Tuendelee na 2) usimamizi wa fedha (financial management) 2) usimamizi wa fedha (financial management) Sasa hapa ndipo penyewe, ni hakika tena sana kuwa hakuna mtu ambaye hajapitia hili, kitu kizuri ni kwamba, kwa uzoefu wangu, kadiri unapopata changamoto za kifedha, ndipo unapofahamu namna ya kukabiliana nazo. Usikate tamaa, twende pamoja.... Katika maisha kuna watu wanaingiza kiasi kingi sana cha fedha, kuna watu wanaingiza kiasi cha kati, kuna wanaoingiza kiasi cha chini, wote hawa wanahitaji kuishi, wanahitaji

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI/KIGOMA/GWANJI

Jinsi ya kutengeneza Sabuni ya magadi( gwanji)ama Sabuni ya kigoma. MAHITAJI Caustic Soda kilo 3 Mafuta ya mawese lita 20 Sodium Silicate Maji lita 10 Rangi ya bluu vijiko 3 Jinsi ya kutengeneza. 1)Chukuwa coustic soda changanya na maji na uanze kukoroga kuelekea upande mmoja endelea kufanya hivyo hadi vichanganyikane vizur baada ya hapo iache kwa saa 24 2)Chukuwa kindoo kidogo na upunguze mafuta lita 3 kwa ajili ya kuweka rangi pembeni,weka rangi vijiko 3 ,changanya na mafuta uliyopunguza lita 3 kisha koroga mpaka yachanganyikane vizur kabisa 3)Chukuwa coustic soda uliyoloweka kwenye ndoo kubwa ,kisha tia mafuta na uendelee kukoroga kuekekea upande mmoja kwa nguvu na kwa haraka,tia sodium silgett kwa kunyunyuzia kidogo kidogo, endelea kukoroga hadi vichanganyikane viwe kitu kimoja 4)Baada ya hapo andaa ndoo nyingine ndogo ,chukuwa uji uliokoroga au mkorogo wako kias kwa ajili ya kuchanganya na rangi mwanzo na mafuta kisha koroga kwa pamoja vichanganyikane vizur

MAMBO YA KUZINGATIA KATKA KUINUA BIASHARA YAKO NDOGO

“*MAMBO YA KUZINGATIA KUINUA BIASHARA YAKO NDOGO.”* 1. Acha Kulinganisha biashara yako na biashara zingine (Mind your own business).Ukiwa hatua zako ndogo kabisa katika biashara ambayo unaifanya na ukawa mtu wa kulinganisha biashara yako na watu wengine ambao unakuta tayari wameshafika sehemu flani kubwa katika biashara zao hii itakusababisha kuanza kudharau biashara yako na kuona kama haifai. Penda biashara unayoifanya na heshimu sana pale ulipo usiwe na tamaa kuwa juu wakati chini penyewe hujapamaliza.Jifunze kwa wengine lakini heshimu nafasi yako ya sasa. 2. Weka malengo katika biashara yako.Bila malengo katika biashara yako unaweza kubaki hapo hapo ulipo. Hakikisha unapoanza biashara yako uweke malengo kwa kuangalia unataka biashara yako iweje baada ya muda flani na ufanye nini kwa wakati huo ili uweze kusogea katika kutimiza malengo yako hayo mfano umeanza biashara ya 100,000/= na katika malengo yako unataka baada ya mwaka mmoja biashara yako iwe ya mtaji wa 1,000,000/= hapa n

MAMBO YA KUZINGATIA KAMA UNATAKA KUINGIA KWENYE ULIMWENGU WA BIASHARA

*🇹🇿💪USHAURI WA BURE KWA WANAOWAZA KUFANYA BIASHARA*💪 *MAMBO YA KUZINGATIA KAMA UNATAKA KUINGIA KWENYE ULIMWENGU WA BIASHARA* Kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla hujajiingiza kwenye biashara. Nimekuwekea baadhi ya mambo hayo hapa chini. Haya ni yale niliyojifunza on the ground ndani ya miaka yangu michache hii ya ujasiriamali toka mwaka 2011 katika biashara mbali mbali nilizofanya. Ukiyazingatia utaona faida yake. 1. HAKIKISHA UNA ELIMU YA BIASHARA Simaanishi diploma sijui certificate ya chuo au zile notes za Commerce. No.  Hiyo siyo elimu ninayomaanisha. Namaanisha education siyo schooling. Namaanisha aina ya elimu kwa vitendo kama vile apprenticeship. Yaani kujifunza kwa mtu taratibu uone jinsi biashara inavyofanyika. Kama hilo ni gumu kulingana na mazingira basi hakikisha biashara unayotaka kuifanya au mradi unaotaka kuanzisha una watu wanaofanya kitu hicho hicho walio tayari kukupa elimu kila siku hasa miaka miwili ya kwanza katika jambo hilo. Watu watakaokuwa tayari ku

TABIA YA MTU MWENYE NAFASI KUBWA YA KUFIKIA NDOTO YAKE

TABIA YA MTU MWENYE NAFASI KUBWA YA KUFIKIA NDOTO YAKE ____ 🔆 *Mtu anayemcha na kumtegemea mungu*  Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. ~Biblia Kuna watu huwa wana kawaida ya kutenganisha mafanikio na Mungu,watu hawa ni wale wanaotaka vitu kwa njia za mkato . Hawa ndio wale wanajiunga na vyama vya kishetani huku wakisahau kuwa hata shetani alikuwa wa Mungu na baadae akaasi. Mtu mwenye utajiri wa kishetani huwa haudumu.  Mafanikio ya kweli yanatoka kwa Mungu kinyume na hapo twajidanganya wenyewe .Sisi wote tulitokana na Mungu na yeye ndiye aijuaye kesho yetu. Ukweli tunajitahidi kupanga mengi lakini Mungu asipoingilia hakuna matokeo yoyote (Bwana asipoijenga nyumba waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure~Biblia) 🔆 *Mtu anayejaribu vitu* Mtu anayejaribu vitu vingi huyu siku moja atafanikiwa .Haikuwa rahisi kwa Thomas Edson kufiki ndoto yake mpaka alipojaribu mara 1000 , lakini mwisho wa siku akafanikisha .