*JINSI YA KUISHI NDOTO ZAKO*
1) MAHUSIANO (Relationships)
Wakati tunaendelea na somo hili, naomba kila mtu atulie, akae chini, afumbe macho, atafakari ni kwa namna ipi mahusiano yake na watu wake wa karibu yamechangia yeye kufika hapa alipo, inawezekana ni pazuri ama pabaya kulingana na kila mmoja wetu ana ndoto tofauti na mwingine.
Tafakari kwa kina kisha mwishoni nitakupa nini cha kufanya kusimamia mahusiano yako ili yawe daraja katika kuziishi ndoto zako.
Tuendelee na 2) usimamizi wa fedha (financial management)
2) usimamizi wa fedha (financial management)
Sasa hapa ndipo penyewe, ni hakika tena sana kuwa hakuna mtu ambaye hajapitia hili, kitu kizuri ni kwamba, kwa uzoefu wangu, kadiri unapopata changamoto za kifedha, ndipo unapofahamu namna ya kukabiliana nazo.
Usikate tamaa, twende pamoja....
Katika maisha kuna watu wanaingiza kiasi kingi sana cha fedha, kuna watu wanaingiza kiasi cha kati, kuna wanaoingiza kiasi cha chini, wote hawa wanahitaji kuishi, wanahitaji kuziishi ndoto zao.
Changamoto ni pale unaposhindwa kuweka misingi mizuri ya kusimamia fedha zako. Unakuta mtu anapanga bajeti lakini haifuati, unakuta mtu anahamisha matumizi ya fedha (allocation), bajeti inasema hili na yeye akipata fedha anafanya tofauti. Watu wengine wamekua wanahuruma sana kupita kiasi, wanatoa hata wanakosa wao bajeti ya kufanya ya msingi yanayowezesha kuzalisha fedha nyingine, na kuwasaidia wengine, mwishowe wote wanakua wanahitaji msaada.
Unakuta mwanafunzi wa chuo, anapewa ela ya kujikimu (bumu) lakini matumizi yake ya bumu ni tofauti na malengo yake.
Unakuta mtu anakopa ela ya biashara lakini akishaipata anaibadirishia matumizi, analipia mchango wa harusi😀 (changamoto ya mahusiano hii🤗 unakuta mtu kakopa ela ya biashara na kesho yake anapewa kadi ya mchango wa harusi wa besti yake... patamu hapo, unamkatalia besti au unaikataa biashara🤦🏾♂)
Nidhamu ya matumizi ya fedha inagusa kila mtu, kila taasisi.
Vijana ni muhimu kujipima katika hili ili tuweze kuziishi ndoto zetu.
Wakati tunaendelea na somo, chukua muda tafakari juu ya matumizi mabaya ya fedha, matumizi yasiyokusudiwa, matumizi ya nje ya bajeti, ama matumizi bila bajeti, yalivyopelekea wewe kufikia hapa ulipo...
3) usimamizi wa muda (time management)
Hapa watu wengi ukizungumzia time management watakwambia wao ni mabingwa wa kuwahi darsani, kikao, mkutano n.k.
Wengine wanafikiri time management ni kuzingatia muda wa kuanza na muda wa kumaliza pekee, la hasha!! Ni zaidi ya hivyo.
Usimamizi wa muda unaanzia pale unapochagua nini unafanya, kwanini unafanya, kwa ajili ya nini/nani, kina umuhimu gani, kwa muda gani, nk.
Wenge tunafikiria sana kazi, shule, biashara n.k. kuna watu ni mabingwa wa kukesha wanasoma, wanawahi darasani, wanafungua biashara mapema zaidi, kazini mpaka wanatunukiwa tuzo ya kuwahi; lakini bado hawatoboi!! Bado wanashindwa kuziishi ndoto zao, je umewahi kujiuliza ni kwanini?!!!
Ni muhimu kujiuliza; je katika ratiba zako za siku, wiki, mwezi hata mwaka, Mwenyezi Mungu umetengea muda kwa kiasi gani?!!!... kuna wakati nilikua nasali dakika pungufu ya 3, yaani nikiamka napiga ishara ya msalaba, nikiwa nakula napiga ishara ya msalaba, nikiwa nalala usiku napiga ishara ya msalaba ngoma inakua imeisha. Ukipiga hesabu kwa wiki unampa Mungu masaa mangapi unabaki unaduwaaa.... muda mwingine tunashindwa kutimiza ndoto zetu kwasababu hatumpi Mungu nafasi, tunakua mabingwa wa kupanga mambo, mabingwa wa kutekeleza tena kwa wakati, lakini tunasahau kuwa yuko Mungu anayetubariki, mwenye nguvu na aliye mmiliki wa kila kitu ikiwemo pumzi tunayoringia.
Kuna wakati ili utimize ndoto zako ni lazima uhusishe watu wako wa karibu ulio na mahusiano nao. Mathalani, kwa baba/mama mwenye familia iliyobarikiwa kuwa na watoto, kuziishi ndoto zake anahitaji kuwa na mahusiano mazuri na watoto wake (rejea hoja namba 1) lakini unakuta mzazi huyohuyo hatengi muda wa kukaa na familia yake, watoto wake, yeye yuko busy na kazi, yuko busy na biashara... watoto wakiharibikiwa, wanaanza kumpa stress, anashindwa kutimiza majukumu yake kikamilifu, anashindwa kuziishi ndoto zake.
Wakati tunaenda kujadili hoja ya mwisho ya 4, chukua muda tafakari juu ya muda wako, nani umempa muda wako, anautumia kikamilifu, anatumia muda wako kwa manufaa yako, anakusaidia kutimiza ndoto zako!!! Tafakari juu ya ratiba zako, kipi unafanya, kinakuwezesha kuziishi ndoto zako kwa kiwango gani, alafu ndio uje uanze kujiuliza juu ya kuwahi vikao sasa, jiulize kama unawahi kazini, jiulize kwanini kila siku uwe wa mchelewaji wewe tu, kwanini unakua mzito...
4) information management (usimamizi wa taarifa)
Hili ni tatizo kubwa sana hasa kwa vijana wa leo wa kitanzania.
Nini unasikiliza, nini unapenda kusikia, kipi ukiamini, kwanini uamini, umesikia kwa nani, n.k. ni maswali ambayo yakupasa ujiulize kabla hujaifanyia kazi taarifa yoyote ile.
Wengi tunasikia na kuamini taarifa zisizo za kweli wala zisizo na uhalisia.
Lakini ni muhimu kutafakari kwa kina kuhusu usiri wa taarifa zako muhimu, je nani anapaswa kujua nini na kwanini ajue, sio kila mtu ni wa kujua kila kitu!!!
Kabla hujasambaza taarifa yenye kuweza kuleta tafrani jiulize na utafakari juu ya chanzo cha taarifa ile.
Ni muhimu kujua *"information is power"*
Taarifa yako inaweza kutumika kama silaha dhidi yako!!🤔
Ndio maana unasikia siri za taasisi fulani, siri za serikali, n.k. vivyo hivyo hata kwenye maisha yetu ya kila siku, kila mmoja wetu anatakiwa kulinda taarifa zake, maana ndio kujilinda wewe mwenyewe.
Tukiwa tunaelekea kwenye kupata mjumuisho wa somo tajwa hapo juu, chukua muda kutafakari namna taarifa kuhusu mipango yako, ndoto zako, siri zako, mahusiaono yako, kipato chako, n.k. zilivyochangia kufika hapo ulipo. "Just be honest with yourself"
Mwisho nipende kuchukua nafasi hii, kuwahasa vijana wenzangu kuzingatia mambo 4 tajwa hapo juu.
1) boresha mahusiano na kila mtu. Weka mipaka (limits) kwenye mahusiano yako. Thamini mahusiano yako. Jipambanue kwa hao unaohusiana nao ili wakujue vyema hasa misimamo yako. Hakikisha unaimarisha mahusiano na kutatua changamoto zake maana *"kuanzisha mahusiano ni jambo moja, kutatua changamoto za mahusiano ni jambo jingine"*
2) weka misingi imara ya usimamizi wa fedha. Hakikisha unachopanga ndio unachoanza nacho. Usitumie fedha bila mipango. Fanya yale ya msingi tu. Kumbuka kuwasaidia wenye uhitaji. Huruma ina kiasi pia.
3) hakikisha unampa Mungu muda wa kutosha. Familia ipe muda wa kutosha. Fanya kazi sana, tumia muda wako kukuingizia kipato. Thamini muda wako. Mpe muda wako mtu anayeweza kukusaidia kutimiza ndoto zako.
4) linda sana taarifa zako, eleza yale tu machache yanayohitajika, usiwe muongo na mzushi, kuwa *msiri*, sikiliza na fuatilia yenye tija katika kutimiza ndoto zako tu. Pata taarifa sahihi kwenye vyanzo sahihi.
Nakutakia tafakari njema na Mungu akubariki.
Kwa mawasiliano na ushauri tucheki
Email: nyamkaadam@gmail.com
Watsap/call: 0782241723

Comments
Post a Comment