Skip to main content

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI ( MULTI PURPOSE LIQUID SOAP)

*🛑VIFAA MAMA KTK SABUNI YA MAJI*👇🏻ni hivi ndio vinafanya iitwe  sabuni 👇🏻


*Sulphonic acid*
*Sless*
*Rangi*
*Chumvi.*
*Manukato*


*👉Sulphonic acid* kazi yake kubwa ni kuondoa uchafu wa mahali wakati unatumia sabuni, pia inaongeza uzito na povu ktk sabuni yetu, sulphonic acid ikizidishwa ktk sabuni huleta mchubuko wa mikono kea mtumiaji.


*👉Manukato-* kwaajili ya harufu.



*👉Sless( ungarol)*

Kai yake ni kuleta povu, kuongeza uzito, na pia huondoa uchafu wa mahali wakati unapotumia sabuni.



*👉Rangi*
Kuleta rangi ya sabuni pekee.



*👉Chumvi*
Huongeza uzito ktk sabuni, hutunza sabuni isiharibike, pia ikizidishwa hukata sabuni na kuifanya iwe nyepesi Kama maji na kuisha povu.


*🛑Hivi ndio👆🏽 vifaa mama ktk utengenezaji was sabuni ya maji*


*🛑Vifaa vya nyongeza👇🏻*

*📚 Gryselin-* kazi yake kubwa ni kulainisha sabuni na kuzuia michubuko ya ngozi kwa mtumiaji wa sabuni hiyo.



*📚 Formaline-* kazi ya yake kutunza sabuni isiharibike, ila formaline ktk sabuni ya matumizi ya mwilini hatuweki sababu ni dawa Kali inayowekewa maiti pia ili maiti  isiharibike hivyo haishauriwi kutumia kiholela isipokuwa ktk sabuni ya chooni tuu kusudi iue wadudu wasioonekana ktk sink.




*📚Soda ash*
Kazi yake ni kuumua sabuni &  kuongeza uzito, kupunguza ukali wa sulpfonic acid

*CDEA*  Huongeza uzito, povu na kulainisha sabuni iwe smoothly.



📚Hivyo basi unaweza kutengeneza sabuni kwa kutumia vifaa mama pekee na ukatoa sabuni ya kawaida inayofaa kwa matumizi mbali mbali, ama unaweza kuongezea vifaa vya ziada ili *kuboresha sabuni yako zaidi*.

Kanuni za utengenezaji wa sabuni ya maji zipo nyingi, kwa ajili ya kupata kanuni nyingine ambayo utatumia tigna kwaajili ya kuongeza uzito zaidi Hadi sabuni iwe Kama uji tuwasiliane uingie darasani moja kwa moja.

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji nzuri nzito liter 30*

 *√ Malighafi*⬇️


*Maji liter 30.*
   

1• Sulfonic acid 1 litre


2• Sles / Ungarol  1 litre


3•. Soda ash light ½ kg


4• Gryceline  ½ litre


5•. Sodium benzoate  4.5 gram


6•  Cdea  100ml


7•.  Chumvi   1 kg


8•  Tigna 125 gram


9•.   Perfume 50ml


10•   Rangi  gram 2 



*✓Vifaa muhimu*


• Ndoo au Jaba
• Mwiko au mashine
• Gloves
• Miwani
• Koti
• Viatu.
 

*Jinsi ya kutengeneza*


*• Hatua ya 01.*

 Andaa maji lita 30, chota Lita 5 hadi 10 kisha iweke kando, ktk hiyo lita  5 hadi  10 tia tigna 125 gram kisha koroga vizuri hadi upate uji nzito sana kisha weka kando.




*Hatua ya pili*


Chukua sles tia ktk ndoo koroga  tia chumvi kijiko kimoja kuyeyusha sless vizuri, koroga hadi upate cream Kama lotion iwe soft kabisa.



    *Hatua ya tatu*


Chukua Sulfonic acid mimina ktk ndoo yenye sless kisha koroga vizuri na utie maji robo lita ili kulainisha mchanganyiko huo kisha koroga, ongeza soda ash ambayo uliiloweka ktk maji  robo lita itie humo ktk mchanganyiko huo koroga vizuri  ikianza kuleta ugumu anza kutia maji nusu Lita  kisha koroga upate cream soft kabisa



*Hatua ya nne*

Baada ya kupata cream soft endelea kutia maji lita moja moja  hadi lita 19 yaishe huku ukikoroga kuelekea upande mmoja pia maji tia upande ktk ndoo na sio kumwagia katikati ya ndoo,  ongeza chumvi robo tatu ya ile uliyoloweka koroga vizuri kabisa ilete uzito.

*Hatua ya tano*


Baada ya kutia chumvi  ongeza yale maji lita 10 yenye tigna kisha koroga kwa dakika 15,


Tia  gryceline kisha koroga ongeza cdea koroga, ongeza, rangi ambayo uliiloweka,

 Tia rangi kiasi ukitazama isizidi na kukolea saana, iwe rangi kiasi ili kuleta mvuto pia utakoroga kuelekea upande  mmoja ili kuepusha povu kukuzuia kuona ndani.



*Hatua ya tano*

Tia sodium benzoate gram 4.5 kisha koroga vizuri.


Funika sabuni yako iache kwa saa 24 iive kisha utaitia pafyum yako na kuifungasha  tayari kwa matumizi.

Kwa mawasiliano zaidi tucheki kuoitia
0782241723
nyamkaadam@gmail.com
__________________

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA HAIR SHAMPOO

 ▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. 👉MALIGHAFI. 🔸Sless – 1kg. 🔸Cde – 250gm. 🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). 🔸Chumvi -500gm. 🔸Rangi – 5gm. 🔸Perfume – 5gm. 🔸Formaline /citric acid – vijiko 3. 🔸Tigna – 125gm. 🔸Maji – 25lt. 👉VIFAA. 🔹Mwiko. 🔹Beseni. 🔹Mask. 🔹Miwani. 🔹Koti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.  4⃣Chukua maji robo lita  tia  rangi na koroga vizuri kisha  wek

BIASHARA YA JUICE KWA MTAJI MDOGO

 Biashara ya juice ya NANASI + TENDE + NDIMI + TANGAWIZI + ILIKI. NO SUGAR Location: USWAZI MTAJI : 12,000 Ukiweza kuwafurahisha maskini kwa kuwauzia hii juice kwa bei ya chini, tegemea pesa kukufuata kwasababu imeitegenezea njia ije kwako. "Hakuna kitu kigumu katika dunia dhaifu kama kufikiri, pia hakuna kazi yenye mshahara mkubwa kama kufikiri". Mwaka huu jifunze kufikiri vizuri ili ubadilishe maisha yako, kwa kusaidia kuboresha afya za watu wengi wenye pesa kidogo ambao hawezi kuisha kwa gharama siku zote. Kuwa wa kwanza kutatua changamoto za afya zao  kwa kuwapelekea juice yenye virutubisho bora na kusaidia kuboresha afya zao na kupata matokeo mazuri. Haya yote yanahitaji fikra nzuri yenye kuona matatizo ya watu wengi na kutatua. Kiuhalisia hii juice ni ghali sana kwa muonekano kutokana upatikanaji wa bidhaa, ila wewe kuwa wa kwanza kufirikia maskini. Kwenye fikra yako uwe na hii slogan "MASKIN KWANZA", kwa kila biashara unayotaka kuanza kuifanya fikiria maskini