Skip to main content

UMUHIMU WA KUTIMIZA NDOTO YAKO

 *Kwanini ni muhimu kutimiza ndoto yako*

_Kama hujui kwanini unapaswa kutimiza ndoto yako huwezi kufikia ndoto yako. Sababu ndiyo itakusukuma kupambana na kuhakikisha unafikia ndoto yako_ ~

Wewe unayo sababu?

1. *Ndoto Yako Ndio Urithi Mkubwa Wa Kizazi Chako*

_“Utakapokufa na kuiacha familia yako hutaweza kuiachia familia yako kazi yako ya kuajiriwa au mshahara mkubwa unaolipwa sasa”._ ~Joas Yunus

👆👆Kuna uwezekano mkubwa usipoanza kujipanga leo kuiachia familia yako urithi wa ndoto utakayokuwa umetimiza familia yako inaweza kuishi maisha magumu baada ya wewe kutoweka hapa duniani .

Kama ndivyo kuna haja ya kupambana kwa hali na mali utimize ndoto yako ili familia yako ije irithi vitu ulivyoviacha wewe.

Ni bahati mbaya sana watu wengi wanajifikiria wenyewe ndiyo maana mtu akishapata kazi anaridhika na kazi yake na kusahau kuwa nyuma yake kipo kizazi chake kinachomtegemea yeye atengeneze njia .Je, unataka mwanao akimaliza chuo akaombe kazi wapi wakati una uwezo wa kuanza kutengeneza mazingira ya kumuandaa kuwa mkurugenzi wa kampuni utakayoianzisha?

Kama umeajiriwa fanya kazi kwa bidii sana na kuwa bora kazini kwako lakini jambo moja unalopaswa kujua ni kuwa wakati unaendelea kufanya hiyo kazi ya kuajiriwa anza kufikiria nini utaacha hapa duniani ambacho kizazi chako kinaweza kukiendeleza na kunufaika kwacho.

Kifo cha Regnald Abraham Mengi aliyekuwa tajiri mkubwa hapa kwetu Tanzania kilistua watu wengi sana na mimi nikiwa mmoja wao lakini ukweli ni kuwa Mengi amekufa akiwa anaishi kwa kuwa vitu alivyovianzisha kama ndoto yake vitaendelezwa na watu aliowaacha na hasa kizazi chake .

Nyumba uliyowajengea wanao au utakayojenga ni urithi mzuri sana lakini haitoshi kuwa urithi pekee utakaokiachia kizazi chako wakati utakapokuwa umetoweka hapa duniani .Anza kufikiri nini utaacha kwa ajili ya familia yako na kizazi chako kwa ujumla kitakachokuwa alama kubwa na kusaidia watu wengi .

Niliwahi kusikia watoto wa marehemu wakimlaumu marehemu kwa maneno haya marehemu baba yetu alikuwa mtu mkubwa kazini kwake ,aliwahi kupata pesa nyingi sana angekuwa na akili angeanzisha vitu vingi vya kutusaidia lakini alidhani anaishi duniani mwenyewe .Hakufikiri nini kitatokea baada ya yeye kutuacha . Maneno ya watoto hawa wa marehemu yakuachia funzo kubwa ya kutumia vizuri kila nafasi unayoipata .Usiache manunguniko hapa duniani acha sherehe duniani yaani watu washerehekee kuwa umeacha vitu vikubwa duniani .

Niliyafurahia maneno ya Marehemu Ruge Mutahaba aliyomwambia Joseph Kusaga kabla ya kifo chake. Ruge Alisema Nikifa msilie bali fanyeni sherehe. Unadhani Kwanini  Ruge Mutahaba alikuwa na ujasiri wa kutamka maneno hayo ? Bila shaka ni kwa sababu alikuwa amefanya mambo mengi kabla ya kifo chake ambayo yataishi na kuwasaidia watu wengi.

2. *Ndoto Yako Ndiyo Alama Kubwa Utakayoacha Duniani*

👆👆
_“Hutakumbukwa kwa ghorofa kubwa ulilojenga, hutakumbukwa kwa magari ya gharama uliyotembelea lakini utakumbukwa kwa mambo uliyoyoyaasisi na yakawasaidia wengine maana ndoto yako lazima iguse maisha ya wengine.”_

.

👆👆
Siku moja tukiwa tunatoka mochwari kuchukua mwili wa marehemu ndugu mmoja alisema Watu wengi wakishazikwa mara moja wanasahaulika.

 Kauli ya ndugu huyu ilikuwa sahihi kabisa lakini wapo ambao pamoja na kusahaulika mambo ambayo waliyafanya hayataweza kusahaulika .

Mambo yale aliyoyaacha mtu na yanayokumbukwa ndiyo alama alizoacha mtu huyo .Wewe utaacha alama gani?

Rafiki yangu Ushindi Elioth  wakati fulani tukiwa na mazungumzo kama vijana wenye ndoto aliniambia maneno haya Kwa muda mrefu nilielewa kuwa utambulisho wa wa mwanadamu ni alama za vidole lakini baada ya kujifunza na kutafakari sana nikagundua kuwa utambulisho wa mtu haupo katika vitu vinavyoonekana kibaolojia bali katika vile visivyoonekana lakini vikiwa na matokeo makubwa.Tukimtaja Steve Jobs haraka tunakumbuka Apple.Tukimtaja Hayati mwalimu Nyerere tunakumbuka harakati za uhuru wa Tanganyika na vuguvugu la siasa za watu weusi ,Regnilad Mengi  tunakumbuka IPP ,Yesu tunakumbuka wokovu ,Paulo tunakumbuka umisheni wa Ulaya.Likitajwa jina lako tunakumbuka nini ? Alama za vidole? Hasha! .Tutakachokumbuka ni nini ulifanya kwa maisha yako.Ndoto yako itakapotimia itaishi hata baada ya wewe kufa .Ndoto yako si utambulisho peke yake bali pia ni urithi wa dunia utakayoiacha.Timiza ndoto yako ,unayo ,inaishi ndani yako inasubiri uifungue na dunia ifurahie

*3.Ndoto Yako Itawasaidia Wengi"*

_Kutimiza ndoto yako ni kutimiza sababu ya kuwa hapa duniani .Kwa hiyo ndoto yako ni suluhisho kwa wengi hivyo kutimiza ndoto yako ni kusaidia wengi na kutotimiza ni kuwaumiza wengi_ ~Adabert Chenche

👆👆
Ndoto lazima iguse maisha ya watu na kuwasaidia watu.

Ndoto isiyowanufaisha wengine hiyo siyo ndoto.

Kama una ndoto ya kumiliki kampuni utaajiri watu na watu hao utakuwa umegusa maisha yao kwa namna moja au nyingine.

Kama ndoto yako ni kuwa kiongozi, mambo ambayo utayafanya ya kuiletea jamii maendeleo wakati utakapokuwa na dhamana ya uongozi huko ndiko kutakuwa kugusa na kusaidia wengine.

4. *Ndoto Yako Ndiyo Itakupa Furaha Halisi*

_"Ni muhimu mtu kutimiza ndoto yake kwa kuwa itamwezesha mtu huyo kuishi maisha ya mafanikio na akishi ndoto yake anajiamini na kuishi kwa furaha"_
~Sifa Mushi

👆👆
Tafiti zinaonesha kuwa watu wengi hawana furaha na kazi wanazozifanya.

Moja ya sababu za kutokuwa na furaha ni kwa sababu wanafanyia kazi ndoto ya mtu mwingine hivyo siyo rahisi hata kidogo kuwa na furaha.

Kwa asili kila binadamu anapenda uhuru,uhuru huo ndio humpa mtu furaha anayoitaka.

Mshahara mkubwa unaolipwa kwa mwezi hautoshi kukupa furaha wakati hauko huru na kazi yako. Unapokuwa unatumikia ndoto ya mtu mwingine inabidi ufuate ratiba na matakwa ya mwenye ndoto lakini unavyokuwa unatumikia ndoto yako wewe ndiwe unayeratibu kila kitu hivyo unakuwa huru na mwenye furaha.

Sikwambie uache kazi uliyonayo sasa lahasha! bali najaribu kukueleza umuhimu wa kupambana ili ndoto yako siku moja itimie ili uwe na uhuru na furaha katika maisha yako. Maisha ni furaha na furaha unaitafuta mwenyewe hakuna mtu mwingine atakayekupa furaha isipokuwa wewe mwenyewe.

*6.Ndoto Yako Imebeba Kusudi La Kuja Kwako Hapa Duniani*

👆👆
Haukuja duniani kama mzurulaji tu. Hukuumbwa kama nyongeza bali uliumbwa kwa sababu maalumu.

Mungu huangalia sababu kwanza ya kumuumba mtu ndipo anafanya uumbaji.

Wakati Mungu anafanya uumbaji alisema maneno haya;

_"Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."_

👆👆
Ukisoma vizuri maneno hayo yanayozungumzwa na Mungu utaona Kuwa Mungu alimuumba mwanadamu kwa sababu.

*7. Ndoto Yako Ni Hamasa Kubwa Kwa Watu Wengine*

👆👆
_Sisi binadamu ni viumbe wa kuhamasika tuonapo wengine wamefanya kitu hivyo kutimiza ndoto kwa mtu ni hamasa wazi kusaidia wengine waone nao wana uwezo wa kutimiza ndoto zao_


*"8.Maisha Yanaanza Baada Ya Kutimiza Ndoto*"

“Ukitimiza ndoto yako ndipo utahisi umeanza kuishi hapa duniani.

Kabla ya kutimiza ndoto yako utaishi kwa kutapa tapa ukitafuta wapi pa kushika .

Ikitimia ndoto yako, utapata amani na furaha ya kweli ndani ya Moyo wako"

 Email:nyamkaadam@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA HAIR SHAMPOO

 ▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. 👉MALIGHAFI. 🔸Sless – 1kg. 🔸Cde – 250gm. 🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). 🔸Chumvi -500gm. 🔸Rangi – 5gm. 🔸Perfume – 5gm. 🔸Formaline /citric acid – vijiko 3. 🔸Tigna – 125gm. 🔸Maji – 25lt. 👉VIFAA. 🔹Mwiko. 🔹Beseni. 🔹Mask. 🔹Miwani. 🔹Koti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.  4⃣Chukua maji robo lita  tia  rangi na koroga vizuri kisha  wek

BIASHARA YA JUICE KWA MTAJI MDOGO

 Biashara ya juice ya NANASI + TENDE + NDIMI + TANGAWIZI + ILIKI. NO SUGAR Location: USWAZI MTAJI : 12,000 Ukiweza kuwafurahisha maskini kwa kuwauzia hii juice kwa bei ya chini, tegemea pesa kukufuata kwasababu imeitegenezea njia ije kwako. "Hakuna kitu kigumu katika dunia dhaifu kama kufikiri, pia hakuna kazi yenye mshahara mkubwa kama kufikiri". Mwaka huu jifunze kufikiri vizuri ili ubadilishe maisha yako, kwa kusaidia kuboresha afya za watu wengi wenye pesa kidogo ambao hawezi kuisha kwa gharama siku zote. Kuwa wa kwanza kutatua changamoto za afya zao  kwa kuwapelekea juice yenye virutubisho bora na kusaidia kuboresha afya zao na kupata matokeo mazuri. Haya yote yanahitaji fikra nzuri yenye kuona matatizo ya watu wengi na kutatua. Kiuhalisia hii juice ni ghali sana kwa muonekano kutokana upatikanaji wa bidhaa, ila wewe kuwa wa kwanza kufirikia maskini. Kwenye fikra yako uwe na hii slogan "MASKIN KWANZA", kwa kila biashara unayotaka kuanza kuifanya fikiria maskini

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI ( MULTI PURPOSE LIQUID SOAP)

*🛑VIFAA MAMA KTK SABUNI YA MAJI*👇🏻ni hivi ndio vinafanya iitwe  sabuni 👇🏻 *Sulphonic acid* *Sless* *Rangi* *Chumvi.* *Manukato* *👉Sulphonic acid* kazi yake kubwa ni kuondoa uchafu wa mahali wakati unatumia sabuni, pia inaongeza uzito na povu ktk sabuni yetu, sulphonic acid ikizidishwa ktk sabuni huleta mchubuko wa mikono kea mtumiaji. *👉Manukato-* kwaajili ya harufu. *👉Sless( ungarol)* Kai yake ni kuleta povu, kuongeza uzito, na pia huondoa uchafu wa mahali wakati unapotumia sabuni. *👉Rangi* Kuleta rangi ya sabuni pekee. *👉Chumvi* Huongeza uzito ktk sabuni, hutunza sabuni isiharibike, pia ikizidishwa hukata sabuni na kuifanya iwe nyepesi Kama maji na kuisha povu. *🛑Hivi ndio👆🏽 vifaa mama ktk utengenezaji was sabuni ya maji* *🛑Vifaa vya nyongeza👇🏻* *📚 Gryselin-* kazi yake kubwa ni kulainisha sabuni na kuzuia michubuko ya ngozi kwa mtumiaji wa sabuni hiyo. *📚 Formaline-* kazi ya yake kutunza sabuni isiharibike, ila formaline ktk