Skip to main content

MAMBO YA KUZINGATIA KATKA KUINUA BIASHARA YAKO NDOGO

“*MAMBO YA KUZINGATIA KUINUA BIASHARA YAKO NDOGO.”*

1. Acha Kulinganisha biashara yako na biashara zingine (Mind your own business).Ukiwa hatua zako ndogo kabisa katika biashara ambayo unaifanya na ukawa mtu wa kulinganisha biashara yako na watu wengine ambao unakuta tayari wameshafika sehemu flani kubwa katika biashara zao hii itakusababisha kuanza kudharau biashara yako na kuona kama haifai. Penda biashara unayoifanya na heshimu sana pale ulipo usiwe na tamaa kuwa juu wakati chini penyewe hujapamaliza.Jifunze kwa wengine lakini heshimu nafasi yako ya sasa.

2. Weka malengo katika biashara yako.Bila malengo katika biashara yako unaweza kubaki hapo hapo ulipo. Hakikisha unapoanza biashara yako uweke malengo kwa kuangalia unataka biashara yako iweje baada ya muda flani na ufanye nini kwa wakati huo ili uweze kusogea katika kutimiza malengo yako hayo mfano umeanza biashara ya 100,000/= na katika malengo yako unataka baada ya mwaka mmoja biashara yako iwe ya mtaji wa 1,000,000/= hapa ni lazima upange kila siku ufanye nini kuweze kufanya ndoto yako kutimia, lakini pia ni lazima ujue mambo gani unatakiwa kuacha kuyafanya ambayo yatakusukuma chini na usifikie lengo lako ipasavyo.

3. Ijue biashara yako na jiendeleze katika kujua mambo mapya ambayo yatakusaidia kuweza kuongeza ubunifu katika biashara yako ambayo unaifanya. Usilale na kuamka tuu na kwenda kwenye biashara yako,jiulize leo umejifunza nini kipya cha kuongeza katika biashara yako na umegundua nini unatakiwa kupunguza ili uzidi kusonga mbele katika biashara unayoifanya ili izidi kuwa mpya katika macho ya wateja wako lakini hata katika kuwapatia utatuzi.Ukiwa ni mtu wa kubaki vile vile katika biashara yako utakimbiwa na wateja na mwisho wa siku utaanza kuisema biashara yako ni mbaya.

Kuna mambo kama kujua jinsia ya kuongoza mzunguko wa hela katika biashara yako, jinsi ya kumtawala mteja wako na kumfanya wa kudumu, kujua soko jipya kwaajili ya bidhaa yako,kuboresha mbinu za mauzo n.k unapaswa kuvifahamu tenza zaidi.


4. Jitahidi pia kujua washindani wako wanafanya nini haswa wale ambao wako juu yako zaidi. Hii itakusaidia sana kuweza kujua ni mambo gani ambayo unaweza kuyatumia kwa nafasi yako kuweza kupanda juu zaidi ya hapo ulipo, usijifungie tuu ndani na wala usikatae kujua wengine pia wanafanyaje kitu ambacho kinataka kufanana na chako.

Muda mwingine jiongeze fanya uchunguzi kwa kuingia google andika kitu ambacho unataka kujua zaidi kuhusu washindani wako na baada ya hapo andika pembeni mapungufu ambayo umeyaona katika biashara yako ambayo sasa unaweza anza kufanyia kazi pia kujenga silaha ya ushindi tofauti an washindani wako.

5. Mitandao ya kijamii ni sehemu nzuri ya kuweza kutangaza biashara yako, hakikisha unaonekana kwa maana ya kufanya biashara sio unaonekana kwa manufaa ya watu kukuona na wewe upo kwenye mtandao. Kuna mitandao kama facebook, instagram, twitter, linkeldn inanguvu sana kwa wafanyabiashara haswa kuweza kutambulisha biashara yako kwa watu ambao huwajui pika. Nimekuwa nikitumia mitandao hii katika shughuli zangu na nimeona matokeo makubwa sana kwa kipindi kifupi nawe inawezekana hebu tenga muda kwenye kujifunza kutumia mitandao ikufanyie biashara.

Contact: nyamkaadam@gmail.com
Blog: nyamkacollection.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA HAIR SHAMPOO

 ▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. 👉MALIGHAFI. 🔸Sless – 1kg. 🔸Cde – 250gm. 🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). 🔸Chumvi -500gm. 🔸Rangi – 5gm. 🔸Perfume – 5gm. 🔸Formaline /citric acid – vijiko 3. 🔸Tigna – 125gm. 🔸Maji – 25lt. 👉VIFAA. 🔹Mwiko. 🔹Beseni. 🔹Mask. 🔹Miwani. 🔹Koti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.  4⃣Chukua maji robo lita  tia  rangi na koroga vizuri kisha  wek

BIASHARA YA JUICE KWA MTAJI MDOGO

 Biashara ya juice ya NANASI + TENDE + NDIMI + TANGAWIZI + ILIKI. NO SUGAR Location: USWAZI MTAJI : 12,000 Ukiweza kuwafurahisha maskini kwa kuwauzia hii juice kwa bei ya chini, tegemea pesa kukufuata kwasababu imeitegenezea njia ije kwako. "Hakuna kitu kigumu katika dunia dhaifu kama kufikiri, pia hakuna kazi yenye mshahara mkubwa kama kufikiri". Mwaka huu jifunze kufikiri vizuri ili ubadilishe maisha yako, kwa kusaidia kuboresha afya za watu wengi wenye pesa kidogo ambao hawezi kuisha kwa gharama siku zote. Kuwa wa kwanza kutatua changamoto za afya zao  kwa kuwapelekea juice yenye virutubisho bora na kusaidia kuboresha afya zao na kupata matokeo mazuri. Haya yote yanahitaji fikra nzuri yenye kuona matatizo ya watu wengi na kutatua. Kiuhalisia hii juice ni ghali sana kwa muonekano kutokana upatikanaji wa bidhaa, ila wewe kuwa wa kwanza kufirikia maskini. Kwenye fikra yako uwe na hii slogan "MASKIN KWANZA", kwa kila biashara unayotaka kuanza kuifanya fikiria maskini

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI ( MULTI PURPOSE LIQUID SOAP)

*🛑VIFAA MAMA KTK SABUNI YA MAJI*👇🏻ni hivi ndio vinafanya iitwe  sabuni 👇🏻 *Sulphonic acid* *Sless* *Rangi* *Chumvi.* *Manukato* *👉Sulphonic acid* kazi yake kubwa ni kuondoa uchafu wa mahali wakati unatumia sabuni, pia inaongeza uzito na povu ktk sabuni yetu, sulphonic acid ikizidishwa ktk sabuni huleta mchubuko wa mikono kea mtumiaji. *👉Manukato-* kwaajili ya harufu. *👉Sless( ungarol)* Kai yake ni kuleta povu, kuongeza uzito, na pia huondoa uchafu wa mahali wakati unapotumia sabuni. *👉Rangi* Kuleta rangi ya sabuni pekee. *👉Chumvi* Huongeza uzito ktk sabuni, hutunza sabuni isiharibike, pia ikizidishwa hukata sabuni na kuifanya iwe nyepesi Kama maji na kuisha povu. *🛑Hivi ndio👆🏽 vifaa mama ktk utengenezaji was sabuni ya maji* *🛑Vifaa vya nyongeza👇🏻* *📚 Gryselin-* kazi yake kubwa ni kulainisha sabuni na kuzuia michubuko ya ngozi kwa mtumiaji wa sabuni hiyo. *📚 Formaline-* kazi ya yake kutunza sabuni isiharibike, ila formaline ktk