Skip to main content

TABIA YA MTU MWENYE NAFASI KUBWA YA KUFIKIA NDOTO YAKE

TABIA YA MTU MWENYE NAFASI KUBWA YA KUFIKIA NDOTO YAKE
____

🔆 *Mtu anayemcha na kumtegemea mungu*

 Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. ~Biblia

Kuna watu huwa wana kawaida ya kutenganisha mafanikio na Mungu,watu hawa ni wale wanaotaka vitu kwa njia za mkato . Hawa ndio wale wanajiunga na vyama vya kishetani huku wakisahau kuwa hata shetani alikuwa wa Mungu na baadae akaasi. Mtu mwenye utajiri wa kishetani huwa haudumu.

 Mafanikio ya kweli yanatoka kwa Mungu kinyume na hapo twajidanganya wenyewe .Sisi wote tulitokana na Mungu na yeye ndiye aijuaye kesho yetu. Ukweli tunajitahidi kupanga mengi lakini Mungu asipoingilia hakuna matokeo yoyote (Bwana asipoijenga nyumba waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure~Biblia)

🔆 *Mtu anayejaribu vitu*

Mtu anayejaribu vitu vingi huyu siku moja atafanikiwa .Haikuwa rahisi kwa Thomas Edson kufiki ndoto yake mpaka alipojaribu mara 1000 , lakini mwisho wa siku akafanikisha .Leo tunafurahia matokeo mazuri ya majaribio ya Edson. Ukweli ni kwama mtu anayejaribu vitu lazima atafanikiwa, hukumbuki hata huyo ndugu/rafiki/jirani  yako alivyokuwa ni mtu wa kujaribu vitu na sasa amefanikiwa? Anza kuwa mtu wa kujaribu vitu haijalishi unashindwa mara ngapi.

🔆 *Mtu mwenye bidii*

Mtu mwenye bidii mafanikio kwake ni lazima lakini mtu mvivu ajiandae kuajiriwa na mtu mwenye bidii kwa sababu watu wanaopenda kuajiriwa(kutimiza ndoto za wengine) miaka yote ni watu wavivu wasiopenda kuumiza akili,mwili n.k. Kama wewe una bidii mafanikio yako lazima cha msingi endelea kufanya kwa bidii bila kuchoka. Fanya kila kitu kwa bidii kubwa haijalishi huoni matokeo haraka.

🔆 *Mtu mwenye maarifa*

Maarifa aliyonayo mtu ndiyo humsaidia kugundua fursa ambazo watu wengine hawazioni ambazo ndizo zinamfanikisha mtu. Kwani mchezaji anayefunga sana magoli hata kama beki ya wapinzani wake iko imara siri yake ni nini? Siyo uchawi lakini ni kwa sababu maarifa yake yako juu ya mabeki na kwa hiyo hawezi kuzuulika ndivyo ilivyo kwa mtu mwenye maarifa hawezi kuzuilika kutimiza ndoto zake maana anajua namna ya kupenya hata mahali ambapo inaonekana hapana njia ya kupita kabisa.

🔆 *Mtu asiyekata tamaa*
 Mtu asiyekata tamaa lazima atafanikiwa maana kila siku atakuwa anatafuta mpenyo wa kufikia ndoto yake. Hapa ndipo watu wengi wanashindwa na ndiyo maana wengi wanakufa na ndoto zao. Naelewa njiani kuna magumu mengi lakini wale wanaovumilia mpaka mwisho ndio pekee hufanikiwa.


🔆 *Mtu anayesimamia kile anachokiamini*

Rafiki yangu Mwalimu Robison Sisyan  mwandishi  wa makala za kibiashara  wakati fulani akiwa anafundisha kwenye kundi moja la WhatsApp alisema  ili uweze kufanikiwa ni lazima kwanza uwe na uwezo wa kusimamia kile unachokiamini pale ambapo watu wanaweza kukukosoa kwa kuonesha ni namna gani huwezi kufanikiwa."

Huwa iko hivi na kila siku itakuwa hivyo kwamba watu wanaoamini mawazo yao na kuyasimamia ndio wanaofanikiwa bila kukatishwa tamaa wakiamini kuwa siku moja watakuja kufanikiwa kinyume na hapo kama ni mtu wa kusiliza watu wanaokuvunja moyo utakuwa unatwanga maji kwenye kinu,hutafika kokote.

🔆 *Mtu mwenye mahusiano mazuri na watu*

Mahusiano mazuri na watu  ndiyo huleta mafanikio haraka. Mtu mwenye mahusiano mazuri na watu atakuwa na fursa nyingi ambazo zingine huzipata kutokana na mahusiano mazuri aliyojenga. Mtu huyu ni rahisi kusaidiwa pale anapohisi kushindwa. Mtu mwenye mahusiano mabaya na watu si rahisi kufikia kwenye ndoto na mafanikio anayoyataka.

🔆 *Mtu anayejua thamani ya muda*

Mafanikio yako katika muda.Kwa bahati mbaya watu wengi huwa wanatumia muda ovyo ovyo huku wakishau kuwa muda ni mali haupaswi kuchezewa. Watu waliofanikiwa ni watu walio makini sana na matumizi ya muda .Wanajua  kuwa muda hauwezi kujirudia katika maisha kwa maana hiyo wanakuwa makini sana na matumizi ya muda.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA HAIR SHAMPOO

 ▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. 👉MALIGHAFI. 🔸Sless – 1kg. 🔸Cde – 250gm. 🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). 🔸Chumvi -500gm. 🔸Rangi – 5gm. 🔸Perfume – 5gm. 🔸Formaline /citric acid – vijiko 3. 🔸Tigna – 125gm. 🔸Maji – 25lt. 👉VIFAA. 🔹Mwiko. 🔹Beseni. 🔹Mask. 🔹Miwani. 🔹Koti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.  4⃣Chukua maji robo lita  tia  rangi na koroga vizuri kisha  wek

BIASHARA YA JUICE KWA MTAJI MDOGO

 Biashara ya juice ya NANASI + TENDE + NDIMI + TANGAWIZI + ILIKI. NO SUGAR Location: USWAZI MTAJI : 12,000 Ukiweza kuwafurahisha maskini kwa kuwauzia hii juice kwa bei ya chini, tegemea pesa kukufuata kwasababu imeitegenezea njia ije kwako. "Hakuna kitu kigumu katika dunia dhaifu kama kufikiri, pia hakuna kazi yenye mshahara mkubwa kama kufikiri". Mwaka huu jifunze kufikiri vizuri ili ubadilishe maisha yako, kwa kusaidia kuboresha afya za watu wengi wenye pesa kidogo ambao hawezi kuisha kwa gharama siku zote. Kuwa wa kwanza kutatua changamoto za afya zao  kwa kuwapelekea juice yenye virutubisho bora na kusaidia kuboresha afya zao na kupata matokeo mazuri. Haya yote yanahitaji fikra nzuri yenye kuona matatizo ya watu wengi na kutatua. Kiuhalisia hii juice ni ghali sana kwa muonekano kutokana upatikanaji wa bidhaa, ila wewe kuwa wa kwanza kufirikia maskini. Kwenye fikra yako uwe na hii slogan "MASKIN KWANZA", kwa kila biashara unayotaka kuanza kuifanya fikiria maskini

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI ( MULTI PURPOSE LIQUID SOAP)

*🛑VIFAA MAMA KTK SABUNI YA MAJI*👇🏻ni hivi ndio vinafanya iitwe  sabuni 👇🏻 *Sulphonic acid* *Sless* *Rangi* *Chumvi.* *Manukato* *👉Sulphonic acid* kazi yake kubwa ni kuondoa uchafu wa mahali wakati unatumia sabuni, pia inaongeza uzito na povu ktk sabuni yetu, sulphonic acid ikizidishwa ktk sabuni huleta mchubuko wa mikono kea mtumiaji. *👉Manukato-* kwaajili ya harufu. *👉Sless( ungarol)* Kai yake ni kuleta povu, kuongeza uzito, na pia huondoa uchafu wa mahali wakati unapotumia sabuni. *👉Rangi* Kuleta rangi ya sabuni pekee. *👉Chumvi* Huongeza uzito ktk sabuni, hutunza sabuni isiharibike, pia ikizidishwa hukata sabuni na kuifanya iwe nyepesi Kama maji na kuisha povu. *🛑Hivi ndio👆🏽 vifaa mama ktk utengenezaji was sabuni ya maji* *🛑Vifaa vya nyongeza👇🏻* *📚 Gryselin-* kazi yake kubwa ni kulainisha sabuni na kuzuia michubuko ya ngozi kwa mtumiaji wa sabuni hiyo. *📚 Formaline-* kazi ya yake kutunza sabuni isiharibike, ila formaline ktk