Skip to main content

FANYA MAMBO HAYA UKITAKA KUFANIKIWA KTK MAISHA

*🔨🔨NONDO YA WIKI*🔨🔨🔨🔨🔨🔨

Hallow mambo vipi? Ni matumaini yangu kuwa u mzi

1. *NIA THABITI*- Kwanza kabisa inatakiwa uwe na nia thabiti ambayo itakuwezesha kutumia njia mbali mbali ili kufikia malengo yako. Kama waswahili wasemavyo "penye nia pana njia" hivyo ukitaka kufanya kitu hakikisha una nia kweli kweli ili usifanye kwa kujaribu jaribu

2. *JIAMINI UNAWEZA*- Pili amini kwamba ww unaweza na ww ndo mshindi hivyo ukitaka kufanya kitu muhimu zaidi na sema kwamba mimi naweza hiki. Usiangalie watu wengine kwamba mbona flani alifeli kufanya hiki basi na mimi ntafeli no ur wrong jiamini na jione kwamba ww ndo bora zaidi kufanikisha project. Tazama toka ulipozaliwa hadi leo ngazi ngapi umevuka hadi kufika leo hiyo inaonesha kuwa ni mshindi kwa kila ulifanyalo hivyo jiamini ukiamua kufanya kitu unaweza kabisa. Walioweza wana nini na ww ushindwe kwa nini na  ili iwaje yani? *Go* *Go* unaweza usisite

3 *Fanya kitu kilicho ndani ya uwezo wako*- pia jaribu kufanya kitu kilicho ndani ya uwezo wako usitegemee sana kutoka nje. Kwa mfano unalaki mbili hebu anza nayo hiyo hiyo kuizalisha usitegemee kwamba flani aliniahidi atanipa laki nyingine ngoja nisubir anipe ndo ntaanza no unakosea sana hebu anza nayo hiyo hiyo kama itakoea utapewa ya ahadi basi ikukute tayari hii nyingine inajizalisha. Kwa sababu unaweza sema nisubiri niliyoahidiwa mwisho wa siku ukaanza kuipunguza na pesa yako ya mkononi  hadi mwisho wa siku ukaja kujikuta  huna kitu tena. Waswahili husema efu moja yako ya mkononi ni kubwa sana kuliko laki moja ya ahadi

4. *Iheshimu sana pesa*- pia katika safari yako nzima ya utafutaji jitahidi uwe na nidhamu na pesa kwani pesa ukiidharau nayo itakudharau. Kwa mfano unashika laki tatu unasema haka ka laki ntakafanyia nini labda ingekua ingekua milion basi unaamua kula bata inaisha siku nyingine hivyo hivyo mwisho akili inakuja kukaa sawa unakumbuka kwamba yawezekana ungeanza na ile laki tatu ingekuzalishia na ingekufikisha mahali flani mda unakua umeenda. Jitahidi sana kuiheshimu pesa ndugu yangu maana pesa uingiaji wake ni mgumu lakin utokaji wake ni rahisi sana hebu jizuie kufanya manunuzi ya vitu visivyo vya msingi sana utaifurahia pesa baadae. Kubali hata uonekane mshamba leo halafu kesho ukaonekana mjanja

5. *Usipende sana njia za mkato*- katika utafutaji wengi wetu tunataka kupata kubwa ya haraka haraka ambapo inaweza kusababisha ukapoteza hata kidogo ulicho nacho. Kwa mfano mtu anaambiwa kuna fursa mtandaoni unalipa laki tano basi utakua unaingiza laki mbili kila wiki basi kwa kuwa mtu ana shauku ya kuzipata haraka haraka anajoin humo. Baadae akili inakaa sawa anagundua kwamba nimedanganywa mambo hayako kama nilivoambiwa basi inakua ni majuto na pesa yake imeenda. Tuweni makini sana sana ndugu zangu kwa hizi fursa tuzionazo mtandaoni kwa bahat nzuri mimi mwenyewe hakuna online investment ambayo siijui lakini nachoweza kukwambia usije ukaingia mtegoni . Tafuta  kitu cha maana cha kufanyia na pesa yako ukaingiza pesa hata kama ni kidogo lakini iwe uhakika Mungu yupo atakusaidia tu. Kwa leo nimekuandalia hayo tu mpendwa

*Have a nice weekend see u next Time*🙋‍♂️🙋‍♂️🙋‍♂️🙋‍♂️🙋‍♂️🙋‍♂️

Nyamka senior
Email: nyamkaadam@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI ( MULTI PURPOSE LIQUID SOAP)

*🛑VIFAA MAMA KTK SABUNI YA MAJI*👇🏻ni hivi ndio vinafanya iitwe  sabuni 👇🏻 *Sulphonic acid* *Sless* *Rangi* *Chumvi.* *Manukato* *👉Sulphonic acid* kazi yake kubwa ni kuondoa uchafu wa mahali wakati unatumia sabuni, pia inaongeza uzito na povu ktk sabuni yetu, sulphonic acid ikizidishwa ktk sabuni huleta mchubuko wa mikono kea mtumiaji. *👉Manukato-* kwaajili ya harufu. *👉Sless( ungarol)* Kai yake ni kuleta povu, kuongeza uzito, na pia huondoa uchafu wa mahali wakati unapotumia sabuni. *👉Rangi* Kuleta rangi ya sabuni pekee. *👉Chumvi* Huongeza uzito ktk sabuni, hutunza sabuni isiharibike, pia ikizidishwa hukata sabuni na kuifanya iwe nyepesi Kama maji na kuisha povu. *🛑Hivi ndio👆🏽 vifaa mama ktk utengenezaji was sabuni ya maji* *🛑Vifaa vya nyongeza👇🏻* *📚 Gryselin-* kazi yake kubwa ni kulainisha sabuni na kuzuia michubuko ya ngozi kwa mtumiaji wa sabuni hiyo. *📚 Formaline-* kazi ya yake kutunza sabuni isiharibike, ila formaline ...

JINSI YA KUTENGENEZA HAIR SHAMPOO

 ▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. 👉MALIGHAFI. 🔸Sless – 1kg. 🔸Cde – 250gm. 🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). 🔸Chumvi -500gm. 🔸Rangi – 5gm. 🔸Perfume – 5gm. 🔸Formaline /citric acid – vijiko 3. 🔸Tigna – 125gm. 🔸Maji – 25lt. 👉VIFAA. 🔹Mwiko. 🔹Beseni. 🔹Mask. 🔹Miwani. 🔹Koti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.  4⃣Chukua maji robo lita  tia  rangi na korog...

BIASHARA YA KUUZA RASTA NA MAWIGI

BIASHARA YA KUUZA RASTA NA MAWIGI Biashara ya kuuza Rasta na Mawigi kwa bei ya jumla, wengi wanapata shida kuja paka Dar kununua Rasta na Mawigi kwa gharama ya juu, mfanyabiashara akiwa mgeni Dar anatumia gharama kubwa sana kwa kufikia Guest pamoja na Chakula. Kama ukiwai kutoa hii huduma kwa wafanyabiashara wa mikoani ni FURSA kwako na unakuwa umewasaidia kupunguza gharama kubwa na kupata faida kuwa kwao. Ukitaka kufanikiwa katika hii biashara fanya yafuatayo : Tafuta maduka yanayouza RASTA & MAWIGI kwa bei ya chini. Ili uweze kutoa OFA nzuri na kupata wateja wengi wa mikoani na kuwasaidia nao kupata faida kubwa kwa kununua kwako. Fungua Instagram Account; post RASTA & MAWIGI aina mbalimbali na bei zake, kumpa mteja njia nyingi za kuchagua bidhaa anayotaka kwenda kuuza kwa wateja wake. Pia post video za watu waliosuka kwa kutumia bidhaa zako au waliotumia kwa kupiga picha. Tumia Bank Account, kupokea malipo kutoka kwa wateja wako; kwa kutumia bank akaunti utakuwa umejilind...