Jinsi ya kutengeneza Sabuni ya magadi( gwanji)ama Sabuni ya kigoma.
MAHITAJI
Caustic Soda kilo 3
Mafuta ya mawese lita 20
Sodium Silicate
Maji lita 10
Rangi ya bluu vijiko 3
Jinsi ya kutengeneza.
1)Chukuwa coustic soda changanya na maji na uanze kukoroga kuelekea upande mmoja endelea kufanya hivyo hadi vichanganyikane vizur baada ya hapo iache kwa saa 24
2)Chukuwa kindoo kidogo na upunguze mafuta lita 3 kwa ajili ya kuweka rangi pembeni,weka rangi vijiko 3 ,changanya na mafuta uliyopunguza lita 3 kisha koroga mpaka yachanganyikane vizur kabisa
3)Chukuwa coustic soda uliyoloweka kwenye ndoo kubwa ,kisha tia mafuta na uendelee kukoroga kuekekea upande mmoja kwa nguvu na kwa haraka,tia sodium silgett kwa kunyunyuzia kidogo kidogo, endelea kukoroga hadi vichanganyikane viwe kitu kimoja
4)Baada ya hapo andaa ndoo nyingine ndogo ,chukuwa uji uliokoroga au mkorogo wako kias kwa ajili ya kuchanganya na rangi mwanzo na mafuta kisha koroga kwa pamoja vichanganyikane vizur
5)Kishaa andaa box la kukaushia sabuni na mimina mkorogo wako kwenye box ,kisha chukuwa mkorogo wenye rangi na umimine juu kwa stail ya zigzaga kisha pitisha mwiko ili rangi iingie mpaka chini
Baada ya hapo iache kwa saa 24 ili ikauke vizur,kisha itoe na uikate kate sabuni yako
NB :Kama unataka sabun nyingi vipimo vinaongezeka,au kama ni kidogo vipimo vinapungua inategemea na ww mwenyewe una hitaji kiasi gani. Au kwa vipimo zaid wasiliana nasi kwa:
Email: nyamkaadam@gmail.com
Watsap/call 0782241723
Comments
Post a Comment