Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2019

FAIDA ZA KILIMO CHA MIEMBE(MILIOMI 8 KWA EKARI 1 TU)

                              FAIDA ZA KILIMO CHA MIEMBE (MILIONI 8 KWA EKARI 1 TU) Embe ni tunda maarufu na limekuwa likitambulika kama mfalme wa matunda. Matunda ya embe yanatumika yakiwa mabichi au yameiva. Matunda yaliyoiva yanaliwa kama tunda au pia yanaweza kutengenezwa juisi na jam. Embe mbichi hutumika katika kutengeneza achali. Kama ilivyo kwa miparachichi, miembe hukua haraka na haipukutishi majani na hivyo ni mti unaobadilisha mazingira ya mashamba na kuleta hali ya ukijani kwa mwaka mzima. Miti ya miembe ikipandwa kwa mpango mzuri mashambani inasaidia kurekebisha hali ya hewa kwa kupunguza joto, kuvuta mawingu ya mvua, kupunguza kasi ya upepo, kupunguza mmomonyoko wa ardhi na kufyonza hewa ya ukaa. Hivyo Miembe nayo ni miti mizuri kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Miti hii ikipandwa mashambani kwa mpangilio mzuri wakulima wataweza kulima mazao menginena hivyo kujipatia fedha zaidi, matunda na hata kuni. Miembe hus

JUICE INAYOFAA KWA WENYE UZITO MKUBWA

         JUICE KWA WENYE UZITO MKUBWA Wengi wana tengeneza juice za kawaida ambazo anaweza kunywa mtu yoyote yule lakini wakinywa watu wenye uzito mkubwa , uzito unaongezeka kwasababu juice nyingi zinawekwa sukari nyingi na sukari ndio inayoongeza uzito kwenye mwili. Binafsi nimefanya utafiti nimegundua kwamba kuna baadhi ya mchanganyiko wa matunda bila sukari inasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kabisa uzito kwa muda mfupi. Unaweza kuchukua changamoto hii kwa watu wenye uzito mkubwa ukaifanya kuwa FURSA YA BIASHARA kwako, kwa kuwa tengenezea juice ya mchanganyiko wa matunda ambayo yatasaidia kupunguza uzito mkubwa. Juice ya matunda na mboga za majani husaidia kupunguza uzito mkubwa   kwa muda mfupi; Ifuatayo ni mchanganyiko wa juice nya matunda na mboga za majani inayosaidia kupunguza uzito mkubwa mwilini: Juice ya Carrot Changanya carrot, apple na nusu chungwa pamoja na tangawizi kupata radha nzuri inayovutia mdomoni pamoja na kusaidia kutoa sumu y

UKITAKA KUFANIKIWA JIKITE KWENYE KITU KIMOJA

JIKITE KWENYE KITU KIMOJA Ukitaka kufanikiwa kwenye biashara dili na kitu kimoja ambacho unaweka nguvu zako zote na akili yako. Ni rahisi sana kufanya vizuri na bora zaidi kwenye hiyo biashara. Kuna msemo unasema “Ukitaka kuwa nguvu kwenye biashara dili na kitu moja yaan bidhaa au huduma”. Wengi tunafeli kwasababu tunadili na vitu vyingi kwa wakati mmoja , mwisho tunashindwa kutoa huduma bora na kufanya wateja waondoke na kwenda sehemu nyingine. Kwa mfano 1. Cafe, badala ya kuwa na vitu vingi vya kuuza , wewe uza maziwa fresh na mayai ya kienyeji TU. Kwa kufanya hivyo utakuwa bora sana kwenye kutoa huduma kwa kuwa umejikita kwenye vitu vichache. Mfano 2. Viatu vya mtumba, badala ya kuwa aina nyingi ya viatu wewe jikite kwenye aina moja ya viatu ambavyo bei yake iko juu na kila mteja anajua hilo, kingine dili na mkoa mmoja (Target location) kwa kuuza bidhaa yako ili iwe rahisi kudili na wateja wako na iwe rahisi kufanya delivery kwao na kwa wakati. Kingine jua wateja wako ni wak

FAHAMU BIASHARA YA GRAPHIC DESIGNING

WAZO LA BIASHARA HAUNA MTAJI????...FANYA HIVI..!! Unajua kuna kazi nyingi ambazo mtu utaweza Kujiajiri mwenyewe na mtaji wako mkubwa ni MAARIFA /SKILLS!!...wala ata hauhitaji PESA KUANZA BIASHARA.....ila kwakuwa una maarifa ya ilo jambo bhas u aweza tumia Ujuzi wako Kutengeneza Pesa!! Mojawapo ni GRAPHICS DESIGNING / GRAPHICS DESIGNER Hivi unahitaji Pesa kuwa Graphics Designer????....Sio kweli..... Mimi nina rafiki yangu namfahamu alijifunza GRAPHICS DESIGNING Kupitia Youtube na saivi anatengeneza zaidi ya LAKI.1 kwa week....!! Tena ni kazi anayoifanya as a part time uku akiwa na kazi nyingine...... Hapa nazungumzia Anatengeneza LOGO, POSTERS, Business Cards, Covers na ana EDIT PICHA ZA WATU kwa pesa, Ana-EDIT VIDEOS na anatengeneza hadi KATUNI /ANIMATIONS.......na Matangazo mengine mbali mbali.... !! KWANZA TAMBUA MAMBO HAYA.. FAIDA ZA KUJIFUNZA GRAPHICS DESIGNING!!.... 🔰 Ukiwa Grapgics Designer , unaweza Kujiajiri.....Na Ukafanikiwa kabisa kulingana na juhudi na ubun

BIASHARA YA KUUZA RASTA NA MAWIGI

BIASHARA YA KUUZA RASTA NA MAWIGI Biashara ya kuuza Rasta na Mawigi kwa bei ya jumla, wengi wanapata shida kuja paka Dar kununua Rasta na Mawigi kwa gharama ya juu, mfanyabiashara akiwa mgeni Dar anatumia gharama kubwa sana kwa kufikia Guest pamoja na Chakula. Kama ukiwai kutoa hii huduma kwa wafanyabiashara wa mikoani ni FURSA kwako na unakuwa umewasaidia kupunguza gharama kubwa na kupata faida kuwa kwao. Ukitaka kufanikiwa katika hii biashara fanya yafuatayo : Tafuta maduka yanayouza RASTA & MAWIGI kwa bei ya chini. Ili uweze kutoa OFA nzuri na kupata wateja wengi wa mikoani na kuwasaidia nao kupata faida kubwa kwa kununua kwako. Fungua Instagram Account; post RASTA & MAWIGI aina mbalimbali na bei zake, kumpa mteja njia nyingi za kuchagua bidhaa anayotaka kwenda kuuza kwa wateja wake. Pia post video za watu waliosuka kwa kutumia bidhaa zako au waliotumia kwa kupiga picha. Tumia Bank Account, kupokea malipo kutoka kwa wateja wako; kwa kutumia bank akaunti utakuwa umejilind

BIASHARA ZA MTAJI MDOGO KUANZIA SH.ELFU 10 HADI ELFU 50

BIASHARA ZA MTAJI MDOGO KUANZIA ELFU 10 HADI ELFU 50 1. DAGAA WA BUKOBA Dagaa hawa wanapatikana masoko mengi, hawa wanakua hawana mchanga kabisa, wanauzwa kg moja elfu nane huwa inashuka had elfu tano, hawa unanunua vifuko unapack unauza mtaani kifuko buku Kwenye kilo moja unaweza toa vifuko 15 sawa na elfu kumi na tano so elfu mbili vifuko elfu tano faida. Pia unaweza uza dagaa wa kigoma, zanzibar au mwanza waliokangwa 2. BIASHARA YA MATUNDA Siku hzi watu wengi hasa maofisini wanapenda kula matunda andaa kwa usfi matund yako hapa unaweza tumia elfu kumi na tano, Unanunua matunda mchanganyiko tikiti, ndizi, tango, karoti, papai, parachichi matunda ya elfu kumi na tano buguruni au stereo ni mzigo nunua vifungashio vile vya kuwekea matunda pack matunda yako ambapo yakiuzika vyema unaondoka na faida nusu kwa nusu 3. JUICE ZA MATUNDA Matunda ya elfu kumi waweza toa had lita kumi za juice ambapo lita moja ni sawa na glass tano au nne za juice so kwenye lita kumi upata grass 40 sawa n