JIKITE KWENYE KITU KIMOJA
Ukitaka kufanikiwa kwenye biashara dili na kitu kimoja ambacho unaweka nguvu zako zote na akili yako.
Ni rahisi sana kufanya vizuri na bora zaidi kwenye hiyo biashara. Kuna msemo unasema “Ukitaka kuwa nguvu kwenye biashara dili na kitu moja yaan bidhaa au huduma”.
Wengi tunafeli kwasababu tunadili na vitu vyingi kwa wakati mmoja , mwisho tunashindwa kutoa huduma bora na kufanya wateja waondoke na kwenda sehemu nyingine.
Kwa mfano 1. Cafe, badala ya kuwa na vitu vingi vya kuuza , wewe uza maziwa fresh na mayai ya kienyeji TU.
Kwa kufanya hivyo utakuwa bora sana kwenye kutoa huduma kwa kuwa umejikita kwenye vitu vichache.
Mfano 2. Viatu vya mtumba, badala ya kuwa aina nyingi ya viatu wewe jikite kwenye aina moja ya viatu ambavyo bei yake iko juu na kila mteja anajua hilo, kingine dili na mkoa mmoja (Target location) kwa kuuza bidhaa yako ili iwe rahisi kudili na wateja wako na iwe rahisi kufanya delivery kwao na kwa wakati.
Kingine jua wateja wako ni wakina nani, wazee , vijana, watoto, wanawake , wanaume, wenye umri xx; ili iwe rahisi kwako kipindi umeamua kuweka tangazo ya fb au insta kwa kulipia , ili tangazo lako liwafikie wahusika tu na kutowafikiwa kila mtu ambao wengine hawataki bidhaa au huduma yako, wengi hapa wanapoteza sana pesa kwa kutangaza bila kutarget wateja husika na biashara zao.
Mfano 3. Biashara ya nguo za mitumba, badala ya kudili na nguo za lika lote, chagua lika la kudil nao , kama watoto, vijana, wazee, wanawake, wanaume pamoja na wahuni hahaha.
Ukiwa na lika ya kudili nalo itakuwa rahisi sana kujua wanataka nguo za aina gani , hicho kitafanya uwe bora sana kwenye biashara yako na kuwa kinara na kuteka soko kwa kuwa unadili na wateja unaowajua wanataka nini.
Mfano 4. Juice Bar, badala ya kutengeneza juice mbalimbali za kila aina, dili na aina moja ya juice ambayo utaiboresha zaidi na kuweka virutubisho vya kila aina ndani yake ili iwe nzuri na yenye tija kwenye afya za wateja wako.
Dili sana na wanaume kwenye upande wa nguvu za kiume, tengeneza juice ambavyo itasaidia ambao hawana nguvu za kiume na kuboresha sector hiyo kwa kutumia juice.
Kuna sehemu kariakoo nilikuja juice ya tende karibu na msikiti wa Idrisa, wanauza juice za aina nyingi nyingi ila kuna juice inafanya nistuke inaitwa MASTER, ikabidi niulize ina mchanganyiko wa vitu gani ndani yake. Jamaa akaniambia kuna muhogo, karanga, na maziwa; nikajua kabisa walengwa ni kina nani kutokana na maelezo ya muuzaji.
Nikajiuliza what if wangekuwa wanadili na juice ya MASTER pekeyake na kuiboresha zaidi, ni wateja wangapi wangekuja kunywa au kuagiza kama oda, jibu ni wengi.
Buni kitu ambacho wengi kitawastua na kuvuta kuja kununua bidhaa au huduma kwako kwa kuwa wanajua kinawasaidia nini kwenye afya zao na kuboresha matatizo waliyo kuwa nao awali.
Jifunze kudil na watu wachache kwanza kabla ya kupanua wigo wa biashara , pia jifunze kudili na kitu kimoja au vitu vichache kwenye ili uwe na nguvu ya kutawala na kufanikiwa zaidi kwenye soko.
“Focus on small ponds”
▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. 👉MALIGHAFI. 🔸Sless – 1kg. 🔸Cde – 250gm. 🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). 🔸Chumvi -500gm. 🔸Rangi – 5gm. 🔸Perfume – 5gm. 🔸Formaline /citric acid – vijiko 3. 🔸Tigna – 125gm. 🔸Maji – 25lt. 👉VIFAA. 🔹Mwiko. 🔹Beseni. 🔹Mask. 🔹Miwani. 🔹Koti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando. 4⃣Chukua maji robo lita tia rangi na koroga vizuri kisha wek
Comments
Post a Comment