FAIDA ZA KILIMO CHA MIEMBE (MILIONI 8 KWA EKARI 1 TU)
Embe ni tunda maarufu na limekuwa likitambulika kama mfalme
wa matunda.
Matunda ya embe yanatumika yakiwa mabichi au yameiva.
Matunda yaliyoiva yanaliwa kama tunda au pia yanaweza kutengenezwa juisi na
jam.
Embe mbichi hutumika katika kutengeneza achali.
Kama ilivyo kwa miparachichi, miembe hukua haraka na
haipukutishi majani na hivyo ni mti unaobadilisha mazingira ya mashamba na
kuleta hali ya ukijani kwa mwaka mzima.
Miti ya miembe ikipandwa kwa mpango mzuri mashambani
inasaidia kurekebisha hali ya hewa kwa kupunguza joto, kuvuta mawingu ya mvua,
kupunguza kasi ya upepo, kupunguza mmomonyoko wa ardhi na
kufyonza hewa ya ukaa.
Hivyo Miembe nayo ni miti mizuri kwa kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi. Miti hii ikipandwa mashambani kwa mpangilio mzuri
wakulima wataweza kulima mazao menginena hivyo kujipatia fedha zaidi, matunda
na hata kuni.
Miembe hustawi sehemu zenye joto la wastani na lenye maji au
mvua za kutosha, hata hivyo miembe haistawi vizuri katika maeneo yeney baridi
kali na mvua nyingi kwa mwaka kwa kuwa inahitaji kipindi cha ukame cha miezi
isiyopungua miwili hadi mitatu ili kuwezesha kutoa maua. Pia miembe hihutaji
udongo wenye kina usio twamisha maji na usio na chumvi chumvi.
Aina za maembe
Zipo aina nyingi za embe, kama vile Apple, Ngowe, Boribo,
Tommy Atkin, Haden, Van Dyke, Sensation, Alphonso, Sabre, Keit, Kent, Peach.
Haya ndiyo maembe yenye soko bora na yanatumiwa kuunganishwa/kubebeshwa
(Grafting).
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI
Ili kupata mazao bora ni muhimu kuzingatia kanuni bora za
kilimo cha maembe hasa kanuni zifuatazo:
1. Kuchagua aina bora
• Chagua aina bora ya kupanda kulingana na mahitaji ya soko.
2. Kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu
• Fanya ukaguzi wa shamba mara kwa mara ili uweze
• kudhibiti wadudu na magonjwa ya matunda kabla madhara
hayajawa makubwa
• Ni muhimu kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu ili kupata
mazao bora ambayo yatapata soko zuri na kuweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
• Hakikisha shamba ni safi wakati wote ili kupata matunda
bora na kurahisisha uvunaji.
Matunzo
• Wakati wa mwaka wa kwanza mche unaposhika kwa shamba ni
vyema kuweka kivuli kama ile ya nasari. Pia inasaidia kuweka samadi ili
kuhifadhi unyevu wakati wa kiangazi. Usisahau kupatia miche yako maji ya
kutosha.
• Changanya mazao kama kunde, maharagwe kati ya mistari ili
ardhi itumike ipasavyo.
• Eneo linalozunguka mwembe kama mita moja (1 meter)
lisipandwe mimea ili lisidhuru mti wa miembe.
• Ondoa maua yanayotaka mwanzo baada ya kupandikiza.
Kuota matawi (pruning)
Hii inafanywa ili mti upate mwelekeo uliyo bora wa wakati
mti utakua umekomaa. Ruhusu mti upate tagaa tatu hadi nne (3-4) zinazoelekea
pande tofauti mita moja (1 meter) kutoka chini na zile tagaa zipeane nafasi.
Mara kwa mara mti unapokuwa na tagaa ambazo ni gonjwa,
zimekufa na zinazokingana zahitajika kutolewa. Ili kuwe na hewa ya kutosha
katikati ya matawi.
Kuvuna
• Miche iliyouzwa au kubebeshwa huzaa kuanzia miaka ya tatu
ama nne
• Mwembe mmoja hutoa mtunda 400 – 800 kwa mwaka
Mapato:
Tuangazie makadirio ya Mapato ya Embe.
Ekari 1- inaingia miembe 80 hadi 100 kutegemea na nafasi
(Spacing) iliyotumika.
Tufanye makadirio ya mimea 70 tu ndio iliyofanikiwa kukua na
kutoa matunda
Mti mmoja wa mwembe hutoa matunda 400 hadi 800 kwa
mwaka/msimu. Tuchukue kadirio la chini kabisa la matunda 400
Hivyo Ekari 1= 70 (miti) X 400 (matunda)= 28,000 (matunda)
Bei ya kuuzia shambani ni 300 hadi 600 kwa embe. kutegemea
na aina ya embe na ukubwa wa tunda. Tuchukulie kadirio la chini kabisa la 300
kwa embe.
Ekari 1: matunda 28,000 X 300 = 8,400,000 (milioni 8 na laki
4)
Hichi ni Kipato cha uhakika kwa kila mwaka,ukiwa na ekari 1
tu. Sasa fanya uwe na ekari 5 hadi 10.
Pia kilimo cha Embe hakihitaji ufuatiliaji/usimamizi wa karibu
sana kama ilivyo mazao ya mboga na matunda. Unaweza kuwa busy na shughuli zako
nyingine na bado ukamudu kufanya kilimo hichi cha embe bila stress kabisa na
ukawa unaingiza kipato chako kizuri tu.
Hivyo hichi ni kilimo sahihi kwa wale ambao wanapenda kufanya
kilimo lakini wamebanwa na majukumu mengine.
Comments
Post a Comment