BIASHARA YA KUUZA RASTA NA MAWIGI
Biashara ya kuuza Rasta na Mawigi kwa bei ya jumla, wengi wanapata shida kuja paka Dar kununua Rasta na Mawigi kwa gharama ya juu, mfanyabiashara akiwa mgeni Dar anatumia gharama kubwa sana kwa kufikia Guest pamoja na Chakula.
Kama ukiwai kutoa hii huduma kwa wafanyabiashara wa mikoani ni FURSA kwako na unakuwa umewasaidia kupunguza gharama kubwa na kupata faida kuwa kwao. Ukitaka kufanikiwa katika hii biashara fanya yafuatayo :
Tafuta maduka yanayouza RASTA & MAWIGI kwa bei ya chini. Ili uweze kutoa OFA nzuri na kupata wateja wengi wa mikoani na kuwasaidia nao kupata faida kubwa kwa kununua kwako.
Fungua Instagram Account; post RASTA & MAWIGI aina mbalimbali na bei zake, kumpa mteja njia nyingi za kuchagua bidhaa anayotaka kwenda kuuza kwa wateja wake. Pia post video za watu waliosuka kwa kutumia bidhaa zako au waliotumia kwa kupiga picha.
Tumia Bank Account, kupokea malipo kutoka kwa wateja wako; kwa kutumia bank akaunti utakuwa umejilinda na watu wenye nia mbaya na wewe ambao wanaweza kutuma pesa na baadae kusitisha muamala kwa kurudisha pesa kwenye simu zao.
Fungua group la whatsapp kwa customer care, iwe rahisi wateja kuchat na wewe mbele ya wateja wengine, kwa kufanya hivyo utajenga uaminifu kwa wateja wengine ambao hawaja agiza bidhaa kutoka kwako.
Omba ushuhuda kwa mteja aliyepata mzigo wake apost kwenye group la whatsapp, ili kuendelea kuwa nguvu ya kuamini zaidi kufanya biashara na wewe.
Post pia instagram wengine waone zaidi kwa ambao hawapo kwenye group la whatsapp.
Kuwa mwaminifu kwa wateja wako, acha tabia ya utapeli na maneno mengi mdomoni, kuwa mtu tofauti kabsa kama unataka kufanikiwa kwenye hii biashara.
Acha visingizio, mfano nilishindwa kutuma mzigo mvua ilikuwa kubwa, nilienda kwenye msiba, nilienda kumwangalia mgonjwa muhimbili. Ukiwa mtu wa visingizio ukifanikiwa maisha ni BAHATI.
Kuwa FASTA kutuma mzigo pindi tu unapo tumiwa pesa na mteja kama bado mapema peleka mzigo stand kwa kusafirisha.Ukifanya hivyo wateja watakupenda na kukuamini zaidi kwa kuwa unawajari kwa kuwaishia mizigo yao.
Uza bidhaa zako kwa bei ambao wengi watamani kununua kwako na kuvututiwa na bei ya bidhaa zako kwa ujumla. Sahau utajiri wa mapema kwanza, waza kuboresha huduma kwa wateja.
Weka bei ya kutuma mzigo kwenda kwa mteja, jaribu kuongea na kampuni ya mabus husika kuhusu kusafirisha mizigo yako kwenda mikoani.Wape kibaumbele kampuni husika kwamba unafanya nao biashara wao tu kama kampuni na sio wengine ili wakubali bei unayotaka wewe.
Kuwa online muda wote paka saa 6 usiku. Unapokuwa offline muda mwingi unawapa hofu wateja wako ingawa namba zako za simu uliweka kwenye akaunti yako ya instagram.Kuwa tayari kuwa sikiliza wateja muda wote shida zao na kuzitatua kwa wakati.
Jifunze kuongea lugha nzuri na wateja wako, usijibu wateja wako vibaya hata siku moja. Kumbuka mteja yuko sawa siku zote, wewe ni kuwa na busara na kulinda jina la biashara yako.
Ukimjibu mteja mmoja lugha gani, utakuwa umeharibu biashara pamoja na jina kwa ujumla. Wateja waengi wataogopa kufanya kazi na wewe na kukimbia na kwenda kufanya kazi na mtu mwingie. Kwaiyo kuwa makini sana na maneno yako.
“Ukitaka kufanikiwa zaidi katika biashara , kuwa mwaminifu kwa wateja wako”
▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. 👉MALIGHAFI. 🔸Sless – 1kg. 🔸Cde – 250gm. 🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). 🔸Chumvi -500gm. 🔸Rangi – 5gm. 🔸Perfume – 5gm. 🔸Formaline /citric acid – vijiko 3. 🔸Tigna – 125gm. 🔸Maji – 25lt. 👉VIFAA. 🔹Mwiko. 🔹Beseni. 🔹Mask. 🔹Miwani. 🔹Koti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando. 4⃣Chukua maji robo lita tia rangi na koroga vizuri kisha wek
Comments
Post a Comment