Biashara ya Stationary
Biashara ya stationary imekuwa maarufu sana tanzania nzima, wanaofanya wengi wanajua vitu ambavyo wengi wanajua ndo maana wanagawana wateja na baadhi ya waanzilishi wanashindwa na kufunga ofisi.
Wengi wanafanya biashara hii kwa mazoea na sio kwa ubunifu na mwendelezo wa kujifunza zaidi na zaidi na kuwa bora kwenye kazi yake.
Wengi hawajui kubuni kazi mpya zinazotokana na printing, wengi wanatumia PUBLISHER kutengeneza kadi n.k bila kujua kuna kitu kinaitwa ADOBE ILLUSTRATOR, ADOBE PHOTOSHOP, ADOBE FIREWORKS n.k ambazo ukitumia hizo software unatengeneza kadi ambazo utakuwa tofauti kabsa na wengine , ila watu wanapenda vitu virahisi ndo maana hatuon faida kwenye stationary baadae kufunga ofisi na kutafuta biashara zingine.
Kama unataka kufanikiwa kwenye biashara ya stationary fuata hatua zifuatazo bila kuruka:
1. Penda kujifunza zaidi kuhusu huduma zitokanazo na printing. Usipenda rahisi kutoka publisher wengi wanafanya na kufanya wateja wasione utofauti na kwenda stationary ile wanayoiona mbele yao.
2. Kuwa mbunifu. Buni kitu ambacho kitakitofautisha na wengine na kuwe kwenye category mpya ambayo sokoni haipo. Google Google Google ni dizan gani mpya ya kutengeneza kadi kwa sasa.
3. Jifunze kununua vitu online na sio tz. Fanya jitihada yoyote kujua namna ya kununua vitu online ili uwe na sample ambazo wengine hawana. Kuna notebook niona ebay balaa sidhan kama tz vipo.
4. Location: hii ndo kitu sehem muhimu sana kama hizo step za juu umezifuata bila kuruka, tafuta sehemu ambayo ni karibu na chuo kikuu au ofisi za serikali kama manispaa au tra n.k . Hizo sehemu stationary utaipenda au kutafuta sehemu center(katikati ya mji).
5. Usipenda kufanya kazi pekeyako. Tafuta msaidizi au mtaalamu wa ADOBE ili uwe tofauti kwenye dizani kama kadi, vipeperushi .
6. Tengeneza sample zitokanazo na printing weka sehemu inayoonekana ili wateja waoni. Kumbuka wateja hawajui wanachokitaka paka waoneshe, waoneshe uwezo wako kwa vitendo kuwa mtu wa kuwatamanisha vitu vizuri ambavyo unaviona kwa wazungu na sio kwa wabongo.
7. Weka INTERNET kwenye ofisi yako. Hii itawavuta wateja wanaoweka mavitu yao kwenye email na kutaka kuprint iwe rahisi kwao. Hakikisha internet ipo muda wote.
8. Uza vikorokoro kama PROTECTOR, EARPHONE, COVER, FLASH.
9. Uza na movie za kudownload ili kuwavuta zaidi wateja , fanya mpango uwe na cumputer 2 moja ya mambo ya stationary na nyingine ya kudownload movie , hii ya movie weka UBUNTU kuzuia virus.
10. Computer yenye UBUNTU(Windows). Hii ndio computer ambayo mtu akija na kazi yake kwenye flash , ingiza kwanza kwenye ubuntu na kuangalia kama ina virus ili uwatoe na kulinda computer yako ya WINDOWS 10/8/7 isihasirike na virus.
11. Nenda kwa kujiamini maofisin kuomba tenda za kuprint na ku supply rim. Nenda ukiwa umevaa vizuri na kuonekana smart.
Usisahau kushake mkono na mkuu husika wa kitengo hicho na kumkazia macho usoni na kusema “taja jina lako mwisho sema na furaha ya kuonana na wewe”.
Nilijaribu hivyo nilipoenda manispaa flan mjini hapa kwenye meeting ya kutengeneza SOFTWARE. Kumbuka “Confidence talking produce Confidence thinking”. It work for me…
12. INSTAGRAM ACCOUNT ni lazima
“Ukitaka kufanikiwa haraka, ongeza spidi ya kufeli”
Kwa mawasiliano zaidi tucheki #0748491485 au #0655233833
Comments
Post a Comment