▶ HAIR SHAMPOO◀
_______________________
Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea.
▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA.
👉MALIGHAFI.
🔸Sless – 1kg.
🔸Cde – 250gm.
🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml).
🔸Chumvi -500gm.
🔸Rangi – 5gm.
🔸Perfume – 5gm.
🔸Formaline /citric acid – vijiko 3.
🔸Tigna – 125gm.
🔸Maji – 25lt.
👉VIFAA.
🔹Mwiko.
🔹Beseni.
🔹Mask.
🔹Miwani.
🔹Koti.
▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀
1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando.
2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando.
3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.
4⃣Chukua maji robo lita tia rangi na koroga vizuri kisha weka kando.
5⃣Katika maji lita 12 yenye sless, chukua gryceline tia koroga, ongea cde koroga, tia rangi kiasi koroga, tia ule uji wa tigna kisha koroga kwa dk 5-10.
6⃣Kisha tia chumvi kidogo kidogo huku unakoroga, kadiria uzito unaotaka kwa kuongeza maji yaliyobakia kisha ongeza formaline au cetric acid na mwisho tia perfume koroga kidogo na ifunike iive.
✅Baada ya masaa 24 fungasha tayari kwa matumizi.
▶ SHAMPOO YA LAOE VERA◀
Hii ni shampoo yenye virutubisho lishe vya aloe vera. Miongoni mwa vitamin zinazopatikana katika mmea huu ni vitamin B12 na B14 ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa nywele. Hulainisha nywele kwa kuzuia ngozi kukauka, kuponya michubuko, kuzipatia nywele rangi yake na kuzuia nywele kujisokota. Hivyo huzifanya nywele zikue zikiwa zimenyooka na zenye afya.
👉MAHITAJI (LITA 10)
🔹Maji -lita 10.
🔹Juice soft ya aloe vera -200ml.
🔹Cde -200ml.
🔹Gryceline – 100ml.
🔹Sless -1kg.
🔹Perfume – 20ml.
🔹Rangi (kijani) –10ml.
🔹Tigna -100gm.
🔹Measuring cylinders.
🔹Vifaa kinga (mask, gloves, na koti).
🔹Formaline – 10ml.
▶JINSI YA KUTENGENEZA.
1⃣Pima maji lita 10 kwa kutumia measuring cylinder na mimina kwenye chombo cha kuchanganyia.
2⃣Chukua sless 1kg, gryceline 100ml, formaline 10ml, perfume 20ml na cde 200ml.Kisha vichanganye pembeni bila maji hadi vichanganyikane vizuri hadi sless iyeyuke kabisa.
2⃣Weka tigna 100gm kisha koroga tena vizuri hadi iyeyuke vizuri.
3⃣Weka juice yako ya aloe vera na koroga tena vizuri.
4⃣Malizia kwa kuweka rangi yako 10gm (kadiria) na koroga tena hadi ishike vizuri.
▶Acha povu lishuke tayari kwa matumizi.
▶MAELEZO YA MALIGHAFI.
🔸Maji ni kibebeo.
🔸Sless ni kwa ajili ya kuleta povu.
🔸Cde kwa ajili ya kuongeza povu(booster).
🔸Gryceline ni kwa ajili ya kulainisha ngozi.
🔸Formaline – huzia shampoo yako isiharibike haraka pia huondoa uchafu, vumbi, mba na kuuwa bakteria kwenye nywele.
🔸Juice ya aloe vera ni kuzuia ngozi kukauka, kuzuia nywele kujisokota, kuponya michubuko ya ngozi na kulainisha nywele.
🔸Tigna ni kuleta uzito kwenye shampoo yako.
🔸Perfume huleta harufu nzuri.
Rangi huleta muonekano mzuri.
▶MATUMIZI.
👉Shampoo hii ni ya kiwango cha TBS hivyo yafaa kwa matumizi ya nywele aina zote.
Pia unaweza ukachagua virutubisho uvipendavyo na kuweka kwenye shampoo yako. Miongoni mwa virubisho hivyo ni:
▪Avocado /parachichi.
▪Asali/honey.
▪Olive oil.
▪Kiini cha yai la kienyeji.
✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅
0748491485
Imeandaliwa na Nyamka_Enterprises
Naweza pata wapi hizo marighafi za shampoo kwa Dar mfano sless ,formaline
ReplyDeletena perfume ni hizi zetu za kawaida tunazotumia kwenye mwil or zipo special
kwa kutengenezea bidhaa na cde
Fika ofisini kwetu tabata mwananchi utapata malighafi zote......0748491485
Delete