๐๐ฐ๐ณ๐ฐ ๐พ๐จ๐๐ถ ๐ณ๐จ๐ฒ๐ถ ๐ณ๐จ ๐ฉ๐ฐ๐จ๐บ๐ฏ๐จ๐น๐จ ๐ณ๐ฐ๐ญ๐จ๐ต๐ฐ๐ฒ๐ฐ๐พ๐ฌ ๐ฝ๐ฐ๐ป๐ผ ๐ฝ๐๐จ ๐ฒ๐ผ๐๐ฐ๐ต๐ฎ๐จ๐ป๐ฐ๐จ: ๐ท๐จ๐น๐ป 2
Vitu vingine vya kuzingatia wakati unakuja na wazo lako la biashara.
Yes unaweza fungua biashara kutokana na kitu unachokijua mfano Kinyozi ukafungua saluni yako au mpishi ukafungua restaurant yako. Kumbuka kwakua wewe ni mpishi mzuri sio kwamba utafahamu jinisi ya kuendesha restaurant yako vizuri. Kuna mambo mengi ya kuzingatia
Kama unataka biashara endelevu make sure huduma au bidhaa unayouza wateja wako watarudi kwako tena. Inabidi uwe na bidhaa au huduma ambayo wateja wataendelea kununua kwa muda mrefu. Mfano ni bora uwe na kampuni ya kusafisha swimming pool kuliko kua na kampuni ya ujenzi wa pool.
๐น“Fanya kile unachopenda na pesa zitakufuata.”
Nafikiri ushawahi kusikia huu msemo. Mimi nitaweka msistizo tu sio kila unachokipenda kinaweza kua biashara yenye faida. Yes fanya unachokipenda but angalia kama kinaweza kua biashara yenye faida.
Kanuni mojawapo ya kufanikiwa katika kile unachokifanya ni kwa kupenda kile unachokifanya. Unapochagua wazo unalolipenda ni wazi kuwa utalifanya kwa moyo na kwa ufanisi mkubwa hata kama utakutana na changamoto.
๐นChagua wazo unalolifahamu na kulimudu
Watu wengi hufanya kosa la kuchagua wazo la biashara ambalo hawalifahamu vyema au kulimudu. Hii ni kutokana na kuiga, kukosa ubunifu au hata tamaa ya pesa.
Kumbuka ili wazo lifanikiwe ni lazima litekelezwe na mtu anayelifahamu vyema na kulimudu. Kwa mfano unaanzisha biashara ya hoteli huku ukiwa huna maarifa wa ujuzi wowote kuhusu uendeshaji wa hoteli; ni wazi kuwa hutoweza kufanikiwa.
Wataalamu wa biashara wanashauri ili uanze biashara inabidi uwe na Unique Selling Proposition (Utafauti katika soko) Bidhaa zako au huduma ziwe tofauti na washindani wako. Hii ni changamoto na inaweza kukwamisha, sio lazima bidhaa yako au huduma iwe tofauti.
Kuna baadhi ya bidhaa hazina USP, Badala ya kutafuta USP ya huduma au bidhaa yako tafuta jinsi gani utaiuza kiutofauti
Je una ujuzi au resources ambazo zinaweza kukusaidia kufanya wazo lako la biashara kua na faida? Kama hauna jifunze mpaka uwe na ujuzi au uwezo wa kufanya. Mfano nimeona kuna fursa nyingi kwenye graphics design na huna ujuzi huo, jifunze.
๐นZingatia swala la fedha
Kila biashara inahitaji fedha ili kujiendesha. Hivyo hakikisha wazo la biashara unalolichagua utaweza kupata fedha za kutosha ili kulitekeleza.
Lifahamu wazo vyema kabla ya kuamua kulifanyia kazi, fahamu gharama zote zinazohitajika katika kulitekeleza pamoja na faida itakayopatikana. Kwa njia hii utaweza kufanya maamuzi bora zaidi kama wazo linafaa au la.
๐นAngalia uhitaji wa soko
Watu wengi hawafahamu umuhimu wa kuangalia uhitaji wa soko kabla ya kuchagua wazo la biashara. Unapoangalia uhitaji wa soko ni wazi kuwa utachagua wazo la biashara ambalo litauzika.
Tatua tatizo au changamoto ambayo mteja wako mlengwa anayo. Usichague tu wazo kwa sababu ni wazo au wengine wanalifanya, bali hakikisha wazo lako linahitajika sokoni katika wakati husika.
๐นUshindani
Ushindani ni jambo muhimu ambalo kila mtu anayechagua wazo la biashara anatakiwa kulizingatia, kwani kufanikiwa kwenye biashara kunategemea kiwango cha ushindani na jinsi utakavyokabiliana nacho.
Hakikisha unafahamu vyema ushindani kwenye wazo husika na unaweza kuumudu vyema. Hakuna haja ya kuchagua wazo ambalo unashindana na makampuni yaliyoenea ulimwenguni kote wakati wewe ni mjasiriamali unayeanza..
Wazo lako la biashara kabla ya kurukia na kuanza kufanya hakikisha umefanya utafiti wa kutosha na kikubwa umefanya majaribio kadhaa, Kuna njia za kufanya majaribio ya wazo lako la biashara, baadhi nimeelezea hapa
Kama nilivyoeleza hapo awali, uchaguzi wa wazo la biashara unahitaji utulivu na umakini mkubwa.
Usichague wazo kwa kuwa wengine wamelichagua au wengine linawapa faida; bali chagua lile linalokufaa wewe na mazingira yako.
ASANTENI NA MUWE NA SIKU NJEMA
0748491485
Comments
Post a Comment