Skip to main content

JINSI YA KUTENGENEZA HAIR SHAMPOO

 ▶ HAIR SHAMPOO◀

_______________________

Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea.


▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA.


👉MALIGHAFI.


🔸Sless – 1kg.

🔸Cde – 250gm.

🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml).

🔸Chumvi -500gm.

🔸Rangi – 5gm.

🔸Perfume – 5gm.

🔸Formaline /citric acid – vijiko 3.

🔸Tigna – 125gm.

🔸Maji – 25lt.


👉VIFAA.


🔹Mwiko.

🔹Beseni.

🔹Mask.

🔹Miwani.

🔹Koti.


▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀


1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando.


2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando.


3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.


 4⃣Chukua maji robo lita  tia  rangi na koroga vizuri kisha  weka kando.


5⃣Katika maji lita 12 yenye sless, chukua gryceline tia koroga, ongea cde koroga, tia rangi kiasi koroga, tia ule uji wa tigna kisha koroga kwa dk 5-10.


6⃣Kisha tia chumvi kidogo kidogo huku unakoroga, kadiria uzito unaotaka kwa kuongeza maji yaliyobakia kisha ongeza formaline au cetric acid na mwisho tia perfume koroga kidogo na ifunike iive.


✅Baada ya masaa 24 fungasha tayari kwa matumizi.


▶ SHAMPOO YA LAOE VERA◀


Hii ni shampoo yenye virutubisho lishe vya aloe vera. Miongoni mwa vitamin zinazopatikana katika mmea huu ni vitamin B12 na B14 ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa nywele. Hulainisha nywele kwa kuzuia ngozi kukauka, kuponya michubuko, kuzipatia nywele rangi yake na kuzuia nywele kujisokota. Hivyo huzifanya nywele zikue zikiwa zimenyooka na zenye afya.


👉MAHITAJI (LITA 10)


🔹Maji -lita 10.

🔹Juice soft ya aloe vera -200ml.

🔹Cde -200ml.

🔹Gryceline – 100ml.

🔹Sless -1kg.

🔹Perfume – 20ml.

🔹Rangi (kijani) –10ml.

🔹Tigna -100gm.

🔹Measuring cylinders.

🔹Vifaa kinga (mask, gloves, na koti).

🔹Formaline – 10ml.


▶JINSI YA KUTENGENEZA.


1⃣Pima maji lita 10 kwa kutumia measuring cylinder na mimina kwenye chombo cha kuchanganyia.


2⃣Chukua sless 1kg, gryceline 100ml, formaline 10ml, perfume 20ml na cde 200ml.Kisha vichanganye pembeni bila maji hadi vichanganyikane vizuri   hadi sless iyeyuke kabisa.


 2⃣Weka tigna 100gm kisha koroga tena vizuri hadi iyeyuke vizuri.


3⃣Weka juice yako ya aloe vera na koroga tena vizuri.


4⃣Malizia kwa kuweka rangi yako 10gm (kadiria) na koroga tena hadi ishike vizuri.


▶Acha povu lishuke tayari kwa matumizi.


▶MAELEZO YA MALIGHAFI.


🔸Maji ni kibebeo.

🔸Sless ni kwa ajili ya kuleta povu.

🔸Cde kwa ajili ya kuongeza povu(booster).

🔸Gryceline ni kwa ajili ya kulainisha ngozi.

🔸Formaline – huzia shampoo yako isiharibike haraka pia huondoa uchafu, vumbi, mba na kuuwa bakteria kwenye nywele.

🔸Juice ya aloe vera ni kuzuia ngozi kukauka, kuzuia nywele kujisokota, kuponya michubuko ya ngozi na kulainisha nywele.

🔸Tigna ni kuleta uzito kwenye shampoo yako.

🔸Perfume huleta harufu nzuri.

Rangi huleta muonekano mzuri.


▶MATUMIZI.


👉Shampoo hii ni ya kiwango cha TBS hivyo yafaa kwa matumizi ya nywele aina zote.

Pia unaweza ukachagua virutubisho uvipendavyo na kuweka kwenye shampoo yako. Miongoni mwa virubisho hivyo ni:

▪Avocado /parachichi.

▪Asali/honey.

▪Olive oil.

▪Kiini cha yai la kienyeji.

✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅

             0748491485

Imeandaliwa na Nyamka_Enterprises

Comments

  1. Naweza pata wapi hizo marighafi za shampoo kwa Dar mfano sless ,formaline
    na perfume ni hizi zetu za kawaida tunazotumia kwenye mwil or zipo special
    kwa kutengenezea bidhaa na cde

    ReplyDelete
    Replies
    1. Fika ofisini kwetu tabata mwananchi utapata malighafi zote......0748491485

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI ( MULTI PURPOSE LIQUID SOAP)

*🛑VIFAA MAMA KTK SABUNI YA MAJI*👇🏻ni hivi ndio vinafanya iitwe  sabuni 👇🏻 *Sulphonic acid* *Sless* *Rangi* *Chumvi.* *Manukato* *👉Sulphonic acid* kazi yake kubwa ni kuondoa uchafu wa mahali wakati unatumia sabuni, pia inaongeza uzito na povu ktk sabuni yetu, sulphonic acid ikizidishwa ktk sabuni huleta mchubuko wa mikono kea mtumiaji. *👉Manukato-* kwaajili ya harufu. *👉Sless( ungarol)* Kai yake ni kuleta povu, kuongeza uzito, na pia huondoa uchafu wa mahali wakati unapotumia sabuni. *👉Rangi* Kuleta rangi ya sabuni pekee. *👉Chumvi* Huongeza uzito ktk sabuni, hutunza sabuni isiharibike, pia ikizidishwa hukata sabuni na kuifanya iwe nyepesi Kama maji na kuisha povu. *🛑Hivi ndio👆🏽 vifaa mama ktk utengenezaji was sabuni ya maji* *🛑Vifaa vya nyongeza👇🏻* *📚 Gryselin-* kazi yake kubwa ni kulainisha sabuni na kuzuia michubuko ya ngozi kwa mtumiaji wa sabuni hiyo. *📚 Formaline-* kazi ya yake kutunza sabuni isiharibike, ila formaline ...

BIASHARA YA KUUZA RASTA NA MAWIGI

BIASHARA YA KUUZA RASTA NA MAWIGI Biashara ya kuuza Rasta na Mawigi kwa bei ya jumla, wengi wanapata shida kuja paka Dar kununua Rasta na Mawigi kwa gharama ya juu, mfanyabiashara akiwa mgeni Dar anatumia gharama kubwa sana kwa kufikia Guest pamoja na Chakula. Kama ukiwai kutoa hii huduma kwa wafanyabiashara wa mikoani ni FURSA kwako na unakuwa umewasaidia kupunguza gharama kubwa na kupata faida kuwa kwao. Ukitaka kufanikiwa katika hii biashara fanya yafuatayo : Tafuta maduka yanayouza RASTA & MAWIGI kwa bei ya chini. Ili uweze kutoa OFA nzuri na kupata wateja wengi wa mikoani na kuwasaidia nao kupata faida kubwa kwa kununua kwako. Fungua Instagram Account; post RASTA & MAWIGI aina mbalimbali na bei zake, kumpa mteja njia nyingi za kuchagua bidhaa anayotaka kwenda kuuza kwa wateja wake. Pia post video za watu waliosuka kwa kutumia bidhaa zako au waliotumia kwa kupiga picha. Tumia Bank Account, kupokea malipo kutoka kwa wateja wako; kwa kutumia bank akaunti utakuwa umejilind...