👉𝑱𝑰𝑵𝑺𝑰 𝒀𝑨 𝑲𝑼𝑱𝑨 𝑵𝑨 𝑾𝑨𝒁𝑶 𝒁𝑼𝑹𝑰 𝑳𝑨 𝑩𝑰𝑨𝑺𝑯𝑨𝑹𝑨.
Ili kuweza kufanikiwa kwenye biashara unahitaji kuwa na wazo zuri la biashara. Je unajua jinsi ya kupata wazo hilo zuri la biashara?
𝑷𝑨𝑹𝑻 1
Watu wengi wamekuwa wakiniomba ushauri ni wazo gani zuri la biashara ambalo linaweza kuwapatia faida na mafanikio. Ukweli ni kwamba wazo ambalo ni bora kwa mtu fulani linaweza lisiwe bora kwako.
Moja ya sababu zinazofanya biashara nyingi kufa au kutokuendelea ni kuiga, yaani mtu akianza biashara leo baada ya muda unakuta watu wengine wameiga biashara ile ile, wanaifanya eneo lile lile na kwa mbinu zile zile. Hii ni njia rahisi sana ya kushindwa kwenye biashara.
Kuja na wazo la biashara kuna mambo mengi sana ya kuzingatia, hii ni pamoja na upo eneo gani, mkoa gani, elimu yako, watu waliokuzunguka, ujuzi, umri wako, muda, mtaji, resources, njaa yako, kiu ya kufanikiwa, connection, etc
Hivyo hakuna formula moja ambayo utatumia. Hapa chini nimejaribu tu kukupa njia mbali mbali kama muongozo. Unaweza chagua njia yoyote na kuanza nayo.
🔹TUMIA UJUZI ULIO NAO
Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiriwa na ni fundi seremala, kwa nini usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo?
🔹BADILISHA HOBBY YAKO KUWA PESA
Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu hupata mafanikio, kama wewe hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usifundishe watu kuogelea?
Kuna njia mbali mbali unaweza tumia kuanzisha biashara kutokana na hobby yako pitia uzi huu
🔹NUNUA BIASHARA AMBAYO TAYARI IPO
Ukishindwa kabisa kupata wazo zuri unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizi kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua na kuendelea nayo. Kuna vigezo vya kuangalia kabla ya kununua.
🔹NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani, geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenu au maeneo unayo kwenda kustarehe.
-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
-Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirani huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?
-Ni tatizo gani sugu ambalo wewe mwenyewe hua linakusumbua na hujapata solution?
-Ni kitu gani umeona inaweza kua tatizo mbeleni? Mfano kwa sasa watu wanakula junk food bila kuangalia afya zao hili ni tatizo unaweza kuja na solution yake
-Huduma au bidhaa gani inaweza kuokoa pesa/muda wa mteja wako mtarajiwa?
-Huduma gani inaweza rahisisha maisha ya mtu?
🔹ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA WANAHITAJI NINI?
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kadhalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji.
🔹UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza. Fanya utafiti kabla ya kuanza kuuza bidhaa hizi. Mfano miezi miwili mitatu nyuma kuna mafuta ya wanawake yanaitwa Snail yameuzwa sana. Hii ilikua bidhaa nzuri
🔹ANGALIA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna chaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, kitaifa na kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango wakutosha kwa wewe kupata wazo la biashara
🔹COPY BUSINESS IDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copy idea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika
🔹TUMIA NJIA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA BIASHARA
- Maonyesho ya biashara
- Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
- Kwa marafiki.
🔹MITANDAO YA KIJAMII
Watu kwenye mitandao ya kijamii ni rahisi sana kupost kuhusu matatizo na kero zao kuhusu huduma au bidhaa flani. Wachache hua wanafuatilia na kutatua matatizo hayo. Matatizo hayo yanaweza kua chanzo cha wazo bora la biashara.
🔹WEBSITE ZA BIASHARA
Kuna kurasa za Instagram ambazo hua wanauza vitu mbali mbali au mitandao kama ebay, AliExpress, AliBaba, Kikuu, Inalipa, etc pendelea kuitembelea na kuangalia bidhaa zinazouzwa humo ni chanzo kizuri cha mawazo ya biashara
🔹TEMBELEA MASOKO MAKUBWA
Kwa kutembelea masoko makubwa kama Kariakoo na mengine kama hayo. Yanaweza kukufungua akili kufahamu biashara gani ya kufanya. Kwa kuangalia bidhaa aina gani zinatoka au wateja wanazikimbilia.
🔹UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama kuna jamaa nilimuona TBC katengeneza mashine zake za kukunia nazi kwa umeme. Jamaa anauza mashine 300,000 mashine hizo nikakuta kariakoo vijana wanatumia kukunia nazi moja 200. Kwa siku jamaa wanakuna nazi hadi 500
Kama tulivyoona hapo juu hizo ni baadhi tu ya njia unazoweza kuzifanya ukiwa unatafuta wazo la biashra. Kama kunayoyote nimeisahau unawea kuiongezea.
𝙄𝙉𝘼𝙀𝙉𝘿𝙀𝙇𝙀𝘼 𝙋𝘼𝙍𝙏 2.........
Comments
Post a Comment