Skip to main content

COFEE BODY & FACE SCRUB

                  COFFEE BODY & FACE SCRUB


SCRUB YA KAHAWA

_____________


MAHITAJI

____

1.Unga wa kahawa 115gm

2. Sukari ya brown 115gm

3. Mafuta ya nazi/olive oil 65mls

4. Natural vanilla extract ¼ kijiko cha chai(sio lazima)

5. Vitamin E matone 3

6. G-acid powder vijiko 2

7. Rose water vijiko 2

8. Asali vijiko 3 vya chakula

9. rKay solutions vijiko 2 

10. Mdalasini ya unga/manjano vijiko 2

11. Unga wa mchele kidogo.


JINSI YA KUTENGENEZA

________________

🔹Pima unga wa kahawa na sukari kisha changanya au koroga vizuri kwa muda wa dk 10


🔹Ongeza unga wa mchele uliochekechwa kisha changanya vizuri.


🔹Ongeza mafuta ya nazi au Olive oil na koroga vuzuri kwa dk 10 au zaidi ili upate mchanganyiko mlaini/soft


🔹Ongeza Vitamin E,  Vanilla na mdalasini au manjano kisha koroga.


🔹Baada ya hapo ongeza rose water, G-acid powder na rKay solutions kisha koroga tena vizuri mpaka mchanganyiko wako uwe mlaini.


NB: Ikiwa utapenda Scrub yako iwe laini sana isiwe na mikwaruzo unaweza kusaga kahawa, sukari, unga wa mchele na mafuta ya nazi iwe laini zaidi. Kisha uongeze malighafi zilizo bakia.


✅Mpaka hapo Scrub yako itakuwa tayari, ifungashe tayari kwa matumizi ya uso na mwili.


MATUMIZI: Paka usoni na acha kwa dk 30 kisha osha uso kwa maji ya vuguvugu.


▶SCRUB YA KAHAWA KANUNI YA PILI


✍️JINSI YA KUTENGENEZA SCRUB YA KAHAWA 2⃣

________________________


👉MAHITAJI


👉🏻sukari 

👉🏻asali 

👉🏻kahawa 

👉🏻vitamini E

👉🏻coconut oil 

👉🏻jojoba oil 

👉🏻oliver oil 


👉JINSI YA KUTENGENEZA


🍉hatua ya kwanza chukua bakuli lako la plastic na mweko kisha weka sukari yako robo hakikisha chombo chako ni kikavu .


🍉hatua ya pili ukishaweka sukari yako kwenye chombo chako chukua kahawa yako weka changanya vinzuri hadi vichanganyike 


🍉kisha weka asali yako nusu changanya tena hadi uwone mchanganyiko upo vinzuri


🍉kisha weka vitamin E pamoja na coconut oil endelea kuchanganya mchanganyiko wako vinzuri


🍉baada ya hapo weka jojoba oil changanya vinzuri kisha weka oliver oil changanya vinzuri kabisa hadi mchanganyiko uwe kama uji uji .


NB: HII SCRUB HAIWEKWI MAJI .NA SCRUB HII HUDUMU KWA MUDA WA MIEZI SITA TU. KAMA UTAHITAJI IKAE KWA MUDA MREFU BILA YA KUHARIBIKA HAKIKISHA UNAWEKA PRESERVATIVE.


▶FAIDA NA MATUMIZI YA SCRUB HII

________________________

🌺 Inaondoa chunusi na kurudisha ngozi iliyofubaa katika Hali ya usoft na ubora 

 

🌺Inatumika mwili mzima ktk kuzibua matundu ya hewa na kuweka mwili sawa

🌺Kwa wale wenye matatzo ya miguu pia kukakamaa na kuwa migumu inaweka soft na ulaini mzuri wa miguu yako na mikono

🌺Inatumiwa na wanaume na wanawake       

🌺Hungarisha na  kukufanya uteleze  (haichui) 

🌺Huondoa mikunjo kwenye ngozi 

🌺Hupunguza mafuta na  kukuacha murua 


🌺Humsaidia alieathirika na vipodozi vikali                          

 🌺Hiondoa vipele vnavyojitokeza kwenye makalio.

_____0748491485__________

✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI ( MULTI PURPOSE LIQUID SOAP)

*🛑VIFAA MAMA KTK SABUNI YA MAJI*👇🏻ni hivi ndio vinafanya iitwe  sabuni 👇🏻 *Sulphonic acid* *Sless* *Rangi* *Chumvi.* *Manukato* *👉Sulphonic acid* kazi yake kubwa ni kuondoa uchafu wa mahali wakati unatumia sabuni, pia inaongeza uzito na povu ktk sabuni yetu, sulphonic acid ikizidishwa ktk sabuni huleta mchubuko wa mikono kea mtumiaji. *👉Manukato-* kwaajili ya harufu. *👉Sless( ungarol)* Kai yake ni kuleta povu, kuongeza uzito, na pia huondoa uchafu wa mahali wakati unapotumia sabuni. *👉Rangi* Kuleta rangi ya sabuni pekee. *👉Chumvi* Huongeza uzito ktk sabuni, hutunza sabuni isiharibike, pia ikizidishwa hukata sabuni na kuifanya iwe nyepesi Kama maji na kuisha povu. *🛑Hivi ndio👆🏽 vifaa mama ktk utengenezaji was sabuni ya maji* *🛑Vifaa vya nyongeza👇🏻* *📚 Gryselin-* kazi yake kubwa ni kulainisha sabuni na kuzuia michubuko ya ngozi kwa mtumiaji wa sabuni hiyo. *📚 Formaline-* kazi ya yake kutunza sabuni isiharibike, ila formaline ...

BIASHARA YA KUUZA RASTA NA MAWIGI

BIASHARA YA KUUZA RASTA NA MAWIGI Biashara ya kuuza Rasta na Mawigi kwa bei ya jumla, wengi wanapata shida kuja paka Dar kununua Rasta na Mawigi kwa gharama ya juu, mfanyabiashara akiwa mgeni Dar anatumia gharama kubwa sana kwa kufikia Guest pamoja na Chakula. Kama ukiwai kutoa hii huduma kwa wafanyabiashara wa mikoani ni FURSA kwako na unakuwa umewasaidia kupunguza gharama kubwa na kupata faida kuwa kwao. Ukitaka kufanikiwa katika hii biashara fanya yafuatayo : Tafuta maduka yanayouza RASTA & MAWIGI kwa bei ya chini. Ili uweze kutoa OFA nzuri na kupata wateja wengi wa mikoani na kuwasaidia nao kupata faida kubwa kwa kununua kwako. Fungua Instagram Account; post RASTA & MAWIGI aina mbalimbali na bei zake, kumpa mteja njia nyingi za kuchagua bidhaa anayotaka kwenda kuuza kwa wateja wake. Pia post video za watu waliosuka kwa kutumia bidhaa zako au waliotumia kwa kupiga picha. Tumia Bank Account, kupokea malipo kutoka kwa wateja wako; kwa kutumia bank akaunti utakuwa umejilind...

JINSI YA KUTENGENEZA HAIR SHAMPOO

 ▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. 👉MALIGHAFI. 🔸Sless – 1kg. 🔸Cde – 250gm. 🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). 🔸Chumvi -500gm. 🔸Rangi – 5gm. 🔸Perfume – 5gm. 🔸Formaline /citric acid – vijiko 3. 🔸Tigna – 125gm. 🔸Maji – 25lt. 👉VIFAA. 🔹Mwiko. 🔹Beseni. 🔹Mask. 🔹Miwani. 🔹Koti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.  4⃣Chukua maji robo lita  tia  rangi na korog...