Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2021

WAZO LA BIASHARA PART O2

 ๐Ÿ‘‰๐‘ฐ๐‘ณ๐‘ฐ ๐‘พ๐‘จ๐’๐‘ถ ๐‘ณ๐‘จ๐‘ฒ๐‘ถ ๐‘ณ๐‘จ ๐‘ฉ๐‘ฐ๐‘จ๐‘บ๐‘ฏ๐‘จ๐‘น๐‘จ ๐‘ณ๐‘ฐ๐‘ญ๐‘จ๐‘ต๐‘ฐ๐‘ฒ๐‘ฐ๐‘พ๐‘ฌ ๐‘ฝ๐‘ฐ๐‘ป๐‘ผ ๐‘ฝ๐’€๐‘จ ๐‘ฒ๐‘ผ๐’๐‘ฐ๐‘ต๐‘ฎ๐‘จ๐‘ป๐‘ฐ๐‘จ:        ๐‘ท๐‘จ๐‘น๐‘ป 2 Vitu vingine vya kuzingatia wakati unakuja na wazo lako la biashara. Yes unaweza fungua biashara kutokana na kitu unachokijua mfano Kinyozi ukafungua saluni yako au mpishi ukafungua restaurant yako. Kumbuka kwakua wewe ni mpishi mzuri sio kwamba utafahamu jinisi ya kuendesha restaurant yako vizuri. Kuna mambo mengi ya kuzingatia Kama unataka biashara endelevu make sure huduma au bidhaa unayouza wateja wako watarudi kwako tena. Inabidi uwe na bidhaa au huduma ambayo wateja wataendelea kununua kwa muda mrefu. Mfano ni bora uwe na kampuni ya kusafisha swimming pool kuliko kua na kampuni ya ujenzi wa pool. ๐Ÿ”น“Fanya kile unachopenda na pesa zitakufuata.”  Nafikiri ushawahi kusikia huu msemo. Mimi nitaweka msistizo tu sio kila unachokipenda kinaweza kua biashara yenye faida. Yes fanya unachokipenda but angalia kama kinaweza kua biashara yenye faida. Kanuni mojawapo y

JINSI YA KUJA NA WAZO ZURI LA BIASHARA PART 1

 ๐Ÿ‘‰๐‘ฑ๐‘ฐ๐‘ต๐‘บ๐‘ฐ ๐’€๐‘จ ๐‘ฒ๐‘ผ๐‘ฑ๐‘จ ๐‘ต๐‘จ ๐‘พ๐‘จ๐’๐‘ถ ๐’๐‘ผ๐‘น๐‘ฐ ๐‘ณ๐‘จ ๐‘ฉ๐‘ฐ๐‘จ๐‘บ๐‘ฏ๐‘จ๐‘น๐‘จ.  Ili kuweza kufanikiwa kwenye biashara unahitaji kuwa na wazo zuri la biashara. Je unajua jinsi ya kupata wazo hilo zuri la biashara?                ๐‘ท๐‘จ๐‘น๐‘ป 1 Watu wengi wamekuwa wakiniomba ushauri ni wazo gani zuri la biashara ambalo linaweza kuwapatia faida na mafanikio. Ukweli ni kwamba wazo ambalo ni bora kwa mtu fulani linaweza lisiwe bora kwako. Moja ya sababu zinazofanya biashara nyingi kufa au kutokuendelea ni kuiga, yaani mtu akianza biashara leo baada ya muda unakuta watu wengine wameiga biashara ile ile, wanaifanya eneo lile lile na kwa mbinu zile zile. Hii ni njia rahisi sana ya kushindwa kwenye biashara. Kuja na wazo la biashara kuna mambo mengi sana ya kuzingatia, hii ni pamoja na upo eneo gani, mkoa gani, elimu yako, watu waliokuzunguka, ujuzi, umri wako, muda, mtaji, resources, njaa yako, kiu ya kufanikiwa, connection, etc Hivyo hakuna formula moja ambayo utatumia. Hapa chini nimejaribu tu kukupa

COFEE BODY & FACE SCRUB

                  COFFEE BODY & FACE SCRUB SCRUB YA KAHAWA _____________ MAHITAJI ____ 1.Unga wa kahawa 115gm 2. Sukari ya brown 115gm 3. Mafuta ya nazi/olive oil 65mls 4. Natural vanilla extract ¼ kijiko cha chai(sio lazima) 5. Vitamin E matone 3 6. G-acid powder vijiko 2 7. Rose water vijiko 2 8. Asali vijiko 3 vya chakula 9. rKay solutions vijiko 2  10. Mdalasini ya unga/manjano vijiko 2 11. Unga wa mchele kidogo. JINSI YA KUTENGENEZA ________________ ๐Ÿ”นPima unga wa kahawa na sukari kisha changanya au koroga vizuri kwa muda wa dk 10 ๐Ÿ”นOngeza unga wa mchele uliochekechwa kisha changanya vizuri. ๐Ÿ”นOngeza mafuta ya nazi au Olive oil na koroga vuzuri kwa dk 10 au zaidi ili upate mchanganyiko mlaini/soft ๐Ÿ”นOngeza Vitamin E,  Vanilla na mdalasini au manjano kisha koroga. ๐Ÿ”นBaada ya hapo ongeza rose water, G-acid powder na rKay solutions kisha koroga tena vizuri mpaka mchanganyiko wako uwe mlaini. NB: Ikiwa utapenda Scrub yako iwe laini sana isiwe na mikwaruzo unaweza kusaga kahawa, su

JINSI YA KUTENGENEZA HAIR SHAMPOO

 ▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. ๐Ÿ‘‰MALIGHAFI. ๐Ÿ”ธSless – 1kg. ๐Ÿ”ธCde – 250gm. ๐Ÿ”ธGryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). ๐Ÿ”ธChumvi -500gm. ๐Ÿ”ธRangi – 5gm. ๐Ÿ”ธPerfume – 5gm. ๐Ÿ”ธFormaline /citric acid – vijiko 3. ๐Ÿ”ธTigna – 125gm. ๐Ÿ”ธMaji – 25lt. ๐Ÿ‘‰VIFAA. ๐Ÿ”นMwiko. ๐Ÿ”นBeseni. ๐Ÿ”นMask. ๐Ÿ”นMiwani. ๐Ÿ”นKoti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.  4⃣Chukua maji robo lita  tia  rangi na koroga vizuri kisha  wek