▶UANDAAJI WA BARAFU ZA MAZIWA
_______________
👉MAHITAJI
🔹CMC 60gm
🔹Maziwa lita 5
🔹Maji lita 5
🔹Sukari 2kg
🔹Rangi vijiko 2
🔹Radha vijiko 2
👉UTENGENEZAJI/UANDAAJI
___________
1. Weka sukari katika sufuria changanya na CMC. Changanya vizuri kwani cmc ina tabia ya kujifunga.
2.Tia maji na koroga vizuri. Baada ya hapo weka maziwa yako lita tano na weka jikoni yachemke.
3.Baada ya hapo epua na acha yapoe.
4.Kisha chuja vizuri mchanganyiko wako
5. Kisha weka rangi na radha uipendayo kisha koroga vizuri.
6. Kisha anza kupaki katika vifuko au vikopo.
7. Weka katika friji ili zigande tayari kwa matumizi.
Comments
Post a Comment