▶FAIDA ZA JUICE YA MAGANDA YA NANASI NA JINSI YA KUIANDAA KAMA TIBA.
_____________________________
NANASI ni tunda lenye ladha nzuri. Mbali na kutumika kama tunda ama juisi yake kutumika kama kinywaji, tunda la nanasi lina faida mbalimbali kwa afya ya mwanadamu.
Baadhi ya faida hizo ni pamoja na :
____________________________
i. UTAJIRI WA VITAMINI NA MADINI :
Nanasi ina vitamini A,B na C na pia ina madini ya chuma, calcium, copper na phosphorous ambayo yote ni muhimu sana katika afya ya mwanadamu.
ii. Tunda hili husaidia kutengeneza damu
iii. Nanasi husaidia kuimarisha mifupa , meno, neva na misuli (muscles).
iv. Tunda la nanasi hutibu matatizo ya tumbo.
v. Hutibu matatizo ya Bandama
vi. Hutibu matatizo ya Ini
vii. Husaidia kusafisha Utumbo mwembamba
viii. Husaidia kutibu Homa
ix. Husaidia kutibu Vidonda mdomoni
x. Husaidia kutibu Magonjwa ya koo
xi. Husaidia kutibu tatizo la Kupoteza kumbukumbu
xii. Husaidia kutibu maradhi ya akili Kukosa mori (low spirit)
xiii. Husaidia kutibu Kikohozi
xiv. Husaidia kutibu tatizo la Kutetemeka
xv. Husaidia kutibu tatizo la Woga ( Anxiety )
xvi. Husaidia kutibu matatizo ya wanawake (upungufu wa hormones au makosa fulani katika sehemu za siri )
xvii. Huondoa shida ya kufunga choo
xviii. Hutibu tatizo la baridi yabisi
xix. Husaidia katika kutibu tatizo la Upungufu wa damu
xx. Pia tunda hili huwasaidia akina mama wanaonyonyesha (uhaba wa maziwa)
▶Jinsi yakutengeneza juisi itokanayo na maganda ya nanasi
_____________________________
```1.Lisafishe nanasi kwa maji safi```
```2.Chonga nanasi lako vizuri kama unavyochonga nanasi la kukata vipande vya matunda, ila wakati huu ukihifadhi maganda yake kwenye chombo safi kama vile sinia, badala ya kuyatupa kwenye ndoo ya uchafu.```
3.Yaweke maganda ya nanasi kwenye sufuria au chungu cha kuchemshia
4.Tia maji ya kutosha kufunika maganda ya mananasi
5.Injika sufuria/chungu jikoni katika moto wa wastani ili ipate moto na kukaribia kuchemsha.
6.Punde tu yanapokuwa yamepata joto la kutosha na kukaribia kuchemka, epua sufuria/chungu toka jikoni.
7.Acha chombo hicho kilivyo na kifunike vizuri kiendelee kupoa, unaweza kuacha hata kwa saa 12 hadi 24 kulingana na hali ya hewa (ukizingatia sana kwenye maeneo ya joto kutokuacha muda mrefu ili isichachuke).
8.Chukua chombo na mimina kwa kuchuja ili kutenganisha juisi na maganda.
9.Gawa juisi kama kinywaji, waweza kuweka barafu kuongeza baridi kadiri ya upendeleo wa mnywaji vile vile unaweza kuongeza asali au sukari kuongeza ladha kadiri ya mtumiaji atakavyo!
ZIADA:
Unaweza kuweka sukari/asali kabla ya kuinjika sufuria/chungu jikoni.
Unaweza kuongeza mdalasini, Iliki au Karafuu kulingana na uhitaji wako. Ni nzuri sana kuandaa juisi kama unajali na unaipenda familia yako. Kuliko kuwanunulia soda za takeaway wanunulie nanasi wajenge afya zao.
Kama umependa weka comment yako hapo chini.
0748491485
nyamka_enterpises
Comments
Post a Comment