Biashara ya juice ya NANASI + TENDE + NDIMI + TANGAWIZI + ILIKI. NO SUGAR
Location: USWAZI
MTAJI : 12,000
Ukiweza kuwafurahisha maskini kwa kuwauzia hii juice kwa bei ya chini, tegemea pesa kukufuata kwasababu imeitegenezea njia ije kwako.
"Hakuna kitu kigumu katika dunia dhaifu kama kufikiri, pia hakuna kazi yenye mshahara mkubwa kama kufikiri".
Mwaka huu jifunze kufikiri vizuri ili ubadilishe maisha yako, kwa kusaidia kuboresha afya za watu wengi wenye pesa kidogo ambao hawezi kuisha kwa gharama siku zote. Kuwa wa kwanza kutatua changamoto za afya zao kwa kuwapelekea juice yenye virutubisho bora na kusaidia kuboresha afya zao na kupata matokeo mazuri.
Haya yote yanahitaji fikra nzuri yenye kuona matatizo ya watu wengi na kutatua.
Kiuhalisia hii juice ni ghali sana kwa muonekano kutokana upatikanaji wa bidhaa, ila wewe kuwa wa kwanza kufirikia maskini.
Kwenye fikra yako uwe na hii slogan "MASKIN KWANZA", kwa kila biashara unayotaka kuanza kuifanya fikiria maskini. Weka kwenye akili yako hii.
Namna ya kuifanya hii biashara ikawe KWELI na sio NDOTO ZA MCHANA , maana ni gharama kuuza hii juice JERO ila wewe UZA kwa ubora ule ule CAFE. HOW?
1. Mforce muuza mananasi akuuzie nanasi moja 500, kivipi kwa kununua mananasi yaliyoiva sana ambayo hayana asubuhi kwa muuzaji. Muuzaji anaogopa hasara lazima hauze chaap.
Muharibu kisaikolojia kwa kumpumbaza na usimpe nafasi ya kufikiri au kuongea, mwambie nanunua mananasi 10 , mpe 5000 na mfuko wa kuyaweka. ALAFU USIACHE KUONGEA 🤣🤣🤣.
2. Tende kilo ni sh 8000, mforce muuzaji akuuzie 10000 kilo 2 kwa kununua tende zilizoiva sana ambazo hazina asubuhi kwako. Fanya kama namba 1.
3. Nunua ndimi, iliki na tangawizi changanya pamoja kwenye BLENDER .
4. Tafuta BLENDER LENYE JAJI LA GLASS , kwasababu kusagia TENDE. Ila kama unaweza kumenya tende sawa unaweza tumia blender ya kawaida. Ila nashauri sana uwe na blender yenye jaji la glass.
5. Usianze na TAKEAWAY itakutafuna sana dili kwa GLASS ZA KUOSHA. ILA UWE MSAFI NA KUJALI MATUMBO YA WANA.
USIWEKE SUGARI ATA TONE. TENDE INASUKARI SANA NA KILO 2 NI SUKARI NYINGI SANA
MBINU YA KIJASUSI KUFANYA BIASHARA HII.
1. Tafuta perfume ambayo ina harufu nzuri ambayo inawastimulate wanaume ukienda kwenye duka la perfume watakwambia. Ila kuwa makini.
2. Penda sana kuvaa nguo nyekundu na njano, ni rangi inayopendwa na watu wengi na macho yanaona haraka sana rangi hizo, wafanya wakukariri.
3. Usipende kuweka pesa kwenye matiti sio poa , tafuta kibeg cha kiunoni kifunge iwe rahisi kuweka pesa na kurudisha chenji.
4. Usipende kabsa kukopesa. Penda cash na usiweke mazoea na wateja. Weka mipaka wa kazi, mazoea weka pembeni. Nawajue upendi mazoea , zaidi ya kutoa huduma tu.
5. Tafuta glass nyembana ndefu, waaminishe wateja kwamba ujazo ni mwingi hainafani na pesa anayotea kwa kumuonesha wala sio kwa kuongea. Ila kiuhalisia ni ujazo mdogo 🤣🤣🤣.
6. Print RED tshirt yenye maneno "UJAZO ZAID NGUVU ZAIDI", wafanye watu wenye wawe na shauku ya kutaka kujua NGUVU ZAIDI? kwenye nini?
7. BAKI NJIA KUU KWENYE RADHA, KWA KUTUMIA VIPIMO, KINYUME NA HAPO MSALA, UTAFUNGA BIASHARA.
8. CHUNYA JUICE KWA CHUJIO LA NASI ILO KURUHUSU ZILE NUTRIENTS WAZPATE WATEJA NA UZITOLEE MAELEZO WAKATI UNAWAPA. NUTRIENTS NI VIRUTUBISHO...
9. Andika umuhimu wa hiyo juice kwenye TSHIRT YAKO KWA NYUMA.
10. BUNI NEMBO YAKO, UANZE KUKUZA BRAND TARATIBU.
11. Ipondee sana sukari ya chai ukiwa nao, sema unauza kitu natural no sugar at all. 🤣🤣🤣
Jifunze kuwa wa kwanza kwenye utekelezaji.
instagram tunapatikana kwa: nyamka_enterprises
Wallah nimejifunza huku nacheka
ReplyDeleteHahahaha hatari
ReplyDeleteWow. Ahsante sana kwa maarifa na ubunifu. Samahani, roughly zinatakiwa kupatikana glass ngapi?
ReplyDeleteNext time ukiwa unatoa elimu kama hii avoid emoj
ReplyDeleteAhsante nimejifunza no sugar at all
ReplyDelete