Skip to main content

NJIA ZA KUPATA MTAJI


Fahamu Njia 8 Unazoweza Kuzitumia ili Kupata Mtaji

Washirikishe Wengine Makala Hii:
Mtaji
Nifanyeje nipate mtaji? Nina wazo zuri lakini sina mtaji? Haya ni maswali ambayo nimekuwa nikiulizwa sana na wasomaji wa Fahamuhili.com, pamoja na watu wengi ninaokutana nao kwenye maisha ya kila siku.
Kutokana na sababu hii, nimeona ni vyema niandae makala ambayo itajibu maswali ya wasomaji wangu pamoja na wale wote wenye maswali kama haya.
Ingawa mtaji siyo kigezo pekee cha kufanikiwa kwenye biashara au mradi unaoufanya, mtaji unabaki kuwa kiungo muhimu sana katika kutekeleza wazo fulani au mradi kwa ufanisi. Kwa kuwa watu wengi huanzisha miradi au biashara kwa lengo la kupata pesa, huwa vigumu sana kuwa na pesa za kutosha kuanza utekelezaji wa wazo hilo.
Karibu ufuatilie makala hii kwa karibu nikushirikishe njia 8 unazoweza kuzitumia ili kupata mtaji wa kutekeleza wazo lako.

1. Akiba binafsi

“Mtu anayeweka akiba, ni mtu anayewaza kuhusu kesho.”
Mara kadhaa nimekuwa nikieleza kuwa kuweka akiba kuna manufaa kemkem, ikiwemo kupata uwezo wa kuwahi fursa mbalimbali na kuzifanyia kazi kwa wakati.
Hivyo basi, unaweza kutunza kiasi fulani cha pesa katika kipato chako hatakama ni kidogo, ili uweze kupata mtaji wa kuanzisha biashara au mradi wako.
Kumbuka! Usitake kuanza biashara na mtaji mkubwa sana kwani kuna hatari ya kuupoteza, jega mtaji wako kidogokidogo; unaweza kuanza na mtaji wa shilingi 10,000 lakini baadaye ukakua na kuwa mamilioni ya pesa. 

2. Kubadilisha mali na vitu binafsi

Nimewahi kukutana na watu kadhaa wakilalamika kuwa hawana mtaji, lakini ukiwachunguza sana utagundua kuwa wamezungukwa na mitaji mikubwa wasiyoitambua.
Hakuna haja yoyote ya kuwa na simu, televisheni, Kompyuta, na nguo za thamani kubwa wakati hauna mtaji wa kutekeleza mradi wako.
Unaweza kuuza vitu vyote ambavyo ukivikosa hutokufa ili uweze kupata mtaji; kumbuka uwekezaji ni muhimu kuliko maisha ya kifahari na anasa.
Ikumbukwe kuwa ukiwekeza utaweza kutengeneza pesa nyingi zaidi na kumudu kununua vitu vingine bora zaidi huko mbeleni.

3. Ndugu na marafiki

Ikiwa una mahusiano mazuri na ndugu zako, wanafamilia au marafiki, kwanini unaona shida kuwaomba wakuwezeshe kupata mtaji?
Andaa wazo vizuri, tafuta watu au marafiki wakaribu watakaokuamini, waombe wakuwezeshe kupata mtaji na uwaahidi utaurejesha mapema kadri uwezavyo ili wakuamini.
Faida za mtaji au mkopo kutoka kwa marafiki na ndugu:
  • Mara nyingi hakuna riba.
  • Hakuna masharti na vigezo vigumu.
  • Upatapo shida katika biashara au mradi wako ni rahisi ndugu kukuelewa.
Kumbuka! Usicheze na mtaji wa biashara au mradi kwa kuwa umeupata kutoka kwa ndugu au marafiki; pia kumbuka kuwa mwaminifu kutimiza mapatano ili wakati mwingine usaidike.

4. Taasisi za kuwezesha wajasiriamali

Hivi leo kuna taasisi na mashirika mbalimbali yanayotoa mitaji ya fedha na vifaa kwa wajasiriamali mbalimbali ili waweze kutekeleza mawazo yao. 
Baadhi ya taasisi hizo ni:
Hivi leo kuna taasisi na mashirika mbalimbali yanayotoa mitaji ya fedha na vifaa kwa wajasiriamali mbalimbali ili waweze kutekeleza mawazo yao. 
Fuatilia vyombo mbalimbali vya habari pia jiunge na vikundi vya wajasiriamali wengine ili zitokeapo fursa za mitaji uweze kuzifahamu na kuzitumia.

5. Mikopo ya taasisi za kifedha

Hivi leo ziko taasisi kedekede zinazotoa mikopo kwa ajili ya watu mbalibali; hivyo, mikopo kutoka kwenye taasisi za kifedha inaweza kutumiwa kama mtaji mzuri sana wa biashara. 
Hata hivyo nimekuwa nikiwashauri wajasiriamali wengi hasa wachanga kutokupendelea njia hii, ikiwa hawajaweka mikakati sahihi ya kutumia na kurejesha mkopo husika.
Hakikisha kama unataka kutumia njia hii kupata mtaji wa biashara au mradi wako, umejipanga vyema na unafahamu wazi njia na mbinu utakazozitumia kurejesha mkopo wa taasisi husika hata kama mambo yatakwenda mrama.

6. Ubia au uwanahisa

Katika dunia yetu ya leo, wapo watu wengi wenye fedha lakini hawajapata mahali pa kuwekeza fedha zao; wengi huwa na pesa nyingi lakini hawana muda wa kuanzisha na kusimamia biashara au mradi.
Unaweza kutumia mbinu hii kupata mtaji, kwa njia ya kuingia ubia au uanahisa na mtu au watu wengine wenye mitaji wanaotafuta mahali pakuiwekeza.
Kwa mfano unaweza kumfuata mtu mwenye pesa na ukamwomba akufungulie biashara au mradi; kisha utampa asilimia fulani ya faida ya biashara au mradi huo kwa kipindi fulani hadi utakapokuwa umereejesha mtaji wake na kiasi fulani cha asante au riba.

7. Mali kauli

Najua umeshajiuliza ‘mali kauli’? Ndiyo, mali kauli ni njia nyingine bora kabisa unayoweza kuitumia kupata mtaji wa biashara kwa kutegemea uaminifu wako.
Zipo biashara kubwa zenye mali nyingi lakini zina mzunguko mdogo katika eneo husika; lakini inawezekana wewe unafahamu mahali ambapo mali hizo zikiuzwa zitauzika vizuri. Unachopaswa kufanya ni kuchukua mali kwenye biashara husika na kwenda kuziuza kisha unarejesha fedha ya mauzo ya bidhaa husika na yule mwenye biashara atakupa gawio fulani kwa kazi hiyo.
Ikiwa utakuwa mwaminifu na kufanya kazi hii kwa bidii, ndani ya muda mfupi utapata mtaji wa kuanzisha biashara yako mwenyewe ambayo imetokana na kuuza mali za biashara nyingine kubwa kwa kuaminika tu (mali kauli).

8. Mashindano

Je, unajua kuna watu wametoka kimaisha kutokana na mitaji waliyoipata kutokana na mashindano mbalimbali? 
Hivi leo, yanaendeshwa mashindano mbalimbali hasa yale yenye lengo la kuibua wajasiriamali wenye mawazo mazuri lakini hawana mtaji. Mfano Mzuri ni Shindano la 3N lililokuwa likiendeshwa na hayati Regnald Mengi lenye lengo la kuwaibua vijana wajasiriamali.
Hivyo basi, unaweza kushiriki mashindano haya, na ukaibuka mshindi na ukajipatia mtaji wa kutosha kutekeleza wazo lako. Kumbuka kuweka nidhamu kwenye pesa unayoipata kwenye mashindano; kwani kutokana na kupatikana kwake bila kutarajia; inaweza kutumiwa vibaya na ik

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA HAIR SHAMPOO

 ▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. 👉MALIGHAFI. 🔸Sless – 1kg. 🔸Cde – 250gm. 🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). 🔸Chumvi -500gm. 🔸Rangi – 5gm. 🔸Perfume – 5gm. 🔸Formaline /citric acid – vijiko 3. 🔸Tigna – 125gm. 🔸Maji – 25lt. 👉VIFAA. 🔹Mwiko. 🔹Beseni. 🔹Mask. 🔹Miwani. 🔹Koti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.  4⃣Chukua maji robo lita  tia  rangi na koroga vizuri kisha  wek

BIASHARA YA JUICE KWA MTAJI MDOGO

 Biashara ya juice ya NANASI + TENDE + NDIMI + TANGAWIZI + ILIKI. NO SUGAR Location: USWAZI MTAJI : 12,000 Ukiweza kuwafurahisha maskini kwa kuwauzia hii juice kwa bei ya chini, tegemea pesa kukufuata kwasababu imeitegenezea njia ije kwako. "Hakuna kitu kigumu katika dunia dhaifu kama kufikiri, pia hakuna kazi yenye mshahara mkubwa kama kufikiri". Mwaka huu jifunze kufikiri vizuri ili ubadilishe maisha yako, kwa kusaidia kuboresha afya za watu wengi wenye pesa kidogo ambao hawezi kuisha kwa gharama siku zote. Kuwa wa kwanza kutatua changamoto za afya zao  kwa kuwapelekea juice yenye virutubisho bora na kusaidia kuboresha afya zao na kupata matokeo mazuri. Haya yote yanahitaji fikra nzuri yenye kuona matatizo ya watu wengi na kutatua. Kiuhalisia hii juice ni ghali sana kwa muonekano kutokana upatikanaji wa bidhaa, ila wewe kuwa wa kwanza kufirikia maskini. Kwenye fikra yako uwe na hii slogan "MASKIN KWANZA", kwa kila biashara unayotaka kuanza kuifanya fikiria maskini

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI ( MULTI PURPOSE LIQUID SOAP)

*🛑VIFAA MAMA KTK SABUNI YA MAJI*👇🏻ni hivi ndio vinafanya iitwe  sabuni 👇🏻 *Sulphonic acid* *Sless* *Rangi* *Chumvi.* *Manukato* *👉Sulphonic acid* kazi yake kubwa ni kuondoa uchafu wa mahali wakati unatumia sabuni, pia inaongeza uzito na povu ktk sabuni yetu, sulphonic acid ikizidishwa ktk sabuni huleta mchubuko wa mikono kea mtumiaji. *👉Manukato-* kwaajili ya harufu. *👉Sless( ungarol)* Kai yake ni kuleta povu, kuongeza uzito, na pia huondoa uchafu wa mahali wakati unapotumia sabuni. *👉Rangi* Kuleta rangi ya sabuni pekee. *👉Chumvi* Huongeza uzito ktk sabuni, hutunza sabuni isiharibike, pia ikizidishwa hukata sabuni na kuifanya iwe nyepesi Kama maji na kuisha povu. *🛑Hivi ndio👆🏽 vifaa mama ktk utengenezaji was sabuni ya maji* *🛑Vifaa vya nyongeza👇🏻* *📚 Gryselin-* kazi yake kubwa ni kulainisha sabuni na kuzuia michubuko ya ngozi kwa mtumiaji wa sabuni hiyo. *📚 Formaline-* kazi ya yake kutunza sabuni isiharibike, ila formaline ktk