Skip to main content

MAMBO 5 MUHIMU YA KUZINGATIA KTK KUCHAGUA ENEO LA BIASHARA

MAMBO 5 MUHIMU YA KUZINGATIA KUCHAGUA ENEO LA BIASHARA
Happy new month wapambanaji. Kama mnavyoona ni mwezi wa 3, siku zinakimbia hatari. Hope mna work hard and smart kutimiza malengo mliyo jiwekea kabla mwaka haujaisha. Leo nitaongelea kitu kimoja muhimu sana kwa mjasiriamali kufahamu.

Ni muhimu kuchagua vizuri eneo au mahali utakapo fanyia Biashara; Kama unavyo jua lengo la Biashara ni kuuza ili upate pesa. Na ili uuze unahitaji watu/ wateja hivyo hakikisha.

1- unachagua eneo utakalo fanyia biashara lina watu wengi wa kutosha, kiasi kwamba utaweza kuuza zaidi na Kwa haraka. Sababu mauzo ya kuwa chini na mzunguko wa Biashara ukiwa mdogo, Biashara itakufa.
.
👇🏿
2- chagua eneo ambalo ni salama kwako na kwa wateja wako, usiweke Biashara yako eneo ambalo lina matukio ya uhalifu, Wizi, ujambazi nk mali zako hakitakuwa salama pia wateja wata ogopa kuja.
.
👇🏿
3- kodi ya pango, chukua frem ambayo una hakika ni nafuu kwako, kwamba kwa mauzo ya biashara yako utaweza kulipa kodi Bila usumbufu, usije jikuta faida yote inaishia kwenye pango wewe hubaki na kitu, ni hasara kubwa.

4- chagua eneo la biashara kulingana na hadhi ya Biashara yako. Bei ya bidhaa zako ni kiashiria cha kwanza kujua umelenga wateja wa kipato gani( kipato cha juu, kati, chini), hivyo weka Biashara yako mahali ambapo itaendana na kipato cha wakazi wa eneo hilo, ambao wataweza kumudu bei ya bidhaa zako. Kinyume na hapo biashara yk itakosa wateja.


5- Eneo linalo fikika muda wote, (majira/vipindi/ msimu), Kwa mfano kipindi cha mvua au masika maeneo mengi yanakuwa ni shida kupitika au kufikika. Hivyo ikiwa Biashara yako wateja watafika kwa vipindi fulani, sio muda wote wa mwaka mzima, mauzo haya takwenda vizuri. Na utakimbiza wateja.
.
Zingatia vitu hivyo 5, uchague location Nzuri kwa Biashara yako uweze kuuza vizuri na kufanikiwa.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA HAIR SHAMPOO

 ▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. 👉MALIGHAFI. 🔸Sless – 1kg. 🔸Cde – 250gm. 🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). 🔸Chumvi -500gm. 🔸Rangi – 5gm. 🔸Perfume – 5gm. 🔸Formaline /citric acid – vijiko 3. 🔸Tigna – 125gm. 🔸Maji – 25lt. 👉VIFAA. 🔹Mwiko. 🔹Beseni. 🔹Mask. 🔹Miwani. 🔹Koti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.  4⃣Chukua maji robo lita  tia  rangi na koroga vizuri kisha  wek

BIASHARA YA JUICE KWA MTAJI MDOGO

 Biashara ya juice ya NANASI + TENDE + NDIMI + TANGAWIZI + ILIKI. NO SUGAR Location: USWAZI MTAJI : 12,000 Ukiweza kuwafurahisha maskini kwa kuwauzia hii juice kwa bei ya chini, tegemea pesa kukufuata kwasababu imeitegenezea njia ije kwako. "Hakuna kitu kigumu katika dunia dhaifu kama kufikiri, pia hakuna kazi yenye mshahara mkubwa kama kufikiri". Mwaka huu jifunze kufikiri vizuri ili ubadilishe maisha yako, kwa kusaidia kuboresha afya za watu wengi wenye pesa kidogo ambao hawezi kuisha kwa gharama siku zote. Kuwa wa kwanza kutatua changamoto za afya zao  kwa kuwapelekea juice yenye virutubisho bora na kusaidia kuboresha afya zao na kupata matokeo mazuri. Haya yote yanahitaji fikra nzuri yenye kuona matatizo ya watu wengi na kutatua. Kiuhalisia hii juice ni ghali sana kwa muonekano kutokana upatikanaji wa bidhaa, ila wewe kuwa wa kwanza kufirikia maskini. Kwenye fikra yako uwe na hii slogan "MASKIN KWANZA", kwa kila biashara unayotaka kuanza kuifanya fikiria maskini

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI ( MULTI PURPOSE LIQUID SOAP)

*🛑VIFAA MAMA KTK SABUNI YA MAJI*👇🏻ni hivi ndio vinafanya iitwe  sabuni 👇🏻 *Sulphonic acid* *Sless* *Rangi* *Chumvi.* *Manukato* *👉Sulphonic acid* kazi yake kubwa ni kuondoa uchafu wa mahali wakati unatumia sabuni, pia inaongeza uzito na povu ktk sabuni yetu, sulphonic acid ikizidishwa ktk sabuni huleta mchubuko wa mikono kea mtumiaji. *👉Manukato-* kwaajili ya harufu. *👉Sless( ungarol)* Kai yake ni kuleta povu, kuongeza uzito, na pia huondoa uchafu wa mahali wakati unapotumia sabuni. *👉Rangi* Kuleta rangi ya sabuni pekee. *👉Chumvi* Huongeza uzito ktk sabuni, hutunza sabuni isiharibike, pia ikizidishwa hukata sabuni na kuifanya iwe nyepesi Kama maji na kuisha povu. *🛑Hivi ndio👆🏽 vifaa mama ktk utengenezaji was sabuni ya maji* *🛑Vifaa vya nyongeza👇🏻* *📚 Gryselin-* kazi yake kubwa ni kulainisha sabuni na kuzuia michubuko ya ngozi kwa mtumiaji wa sabuni hiyo. *📚 Formaline-* kazi ya yake kutunza sabuni isiharibike, ila formaline ktk