Skip to main content

IJUE BIASHARA YA VITENGE

BIASHARA YA VITENGE
⚡️
Inahitaji uwe na wateja wengi (mzunguko wa biashara uwe mkubwa) sababu faida ya vitenge sio kubwa kivile, unahitaji upate wateja wengi uweze kupata faida kubwa (mauzo yawe juu)
⚡️
Tafuta eneo la biashara ambalo wateja wake wanajielewa, lina watu wengi na uza vitu quality bei iwe affordable isimuumize Mteja na wewe upate faida.
⚡️
Jua kuchagua vitenge venye rangi nzuri na vinavyo trend lakini kumbuka kuweka vitenge aina nyingi Mteja awe na choice kubwa.
⚡️
Uwe mchakarikaji, tangaza biashara yako na tafuta wateja, wape wateja wako huduma nzuri ili warudi tena.
⚡️
Usikopeshe, km nilivyo sema faida ni ndogo, ukikopesha hela itakuwa imelala nje, vyote faida na mtaji, biashara hii ni cash tu.
⚡️
Mwanzo ni mgumu usiwe mwepesi kukata tamaa, lazima uwe unatafiti na kujifunza mbinu mpya kila siku, kuboresha biashara yako.
⚡️
Tafuta mafundi nguo wazuri wa kushirikiana nao, wateja ukiwapeleka kwa Fundi akawashonea nguo zao Vizuri wakependeza, kesho atarudi kununua vitenge zaidi na atakuja na mashosti zake.
   By adam nyamka
0782241723

Comments

  1. Nikiwa nafikiria kuanza biashara ya vitenge online

    Nimekutana na makala hi

    Asante Sana 🤝

    ReplyDelete
  2. Naipenda biashara hii ila Sina connection ya vinako patikani kwa Bei nzuri nami niuze jumula

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI ( MULTI PURPOSE LIQUID SOAP)

*🛑VIFAA MAMA KTK SABUNI YA MAJI*👇🏻ni hivi ndio vinafanya iitwe  sabuni 👇🏻 *Sulphonic acid* *Sless* *Rangi* *Chumvi.* *Manukato* *👉Sulphonic acid* kazi yake kubwa ni kuondoa uchafu wa mahali wakati unatumia sabuni, pia inaongeza uzito na povu ktk sabuni yetu, sulphonic acid ikizidishwa ktk sabuni huleta mchubuko wa mikono kea mtumiaji. *👉Manukato-* kwaajili ya harufu. *👉Sless( ungarol)* Kai yake ni kuleta povu, kuongeza uzito, na pia huondoa uchafu wa mahali wakati unapotumia sabuni. *👉Rangi* Kuleta rangi ya sabuni pekee. *👉Chumvi* Huongeza uzito ktk sabuni, hutunza sabuni isiharibike, pia ikizidishwa hukata sabuni na kuifanya iwe nyepesi Kama maji na kuisha povu. *🛑Hivi ndio👆🏽 vifaa mama ktk utengenezaji was sabuni ya maji* *🛑Vifaa vya nyongeza👇🏻* *📚 Gryselin-* kazi yake kubwa ni kulainisha sabuni na kuzuia michubuko ya ngozi kwa mtumiaji wa sabuni hiyo. *📚 Formaline-* kazi ya yake kutunza sabuni isiharibike, ila formaline ...

JINSI YA KUTENGENEZA HAIR SHAMPOO

 ▶ HAIR SHAMPOO◀ _______________________ Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea. ▶ SHAMPOO YA NYWELE NZITO NA BORA. 👉MALIGHAFI. 🔸Sless – 1kg. 🔸Cde – 250gm. 🔸Gryceline – vijiko vitano vya chakula (50ml). 🔸Chumvi -500gm. 🔸Rangi – 5gm. 🔸Perfume – 5gm. 🔸Formaline /citric acid – vijiko 3. 🔸Tigna – 125gm. 🔸Maji – 25lt. 👉VIFAA. 🔹Mwiko. 🔹Beseni. 🔹Mask. 🔹Miwani. 🔹Koti. ▶JINSI YA KIUTENGENEZA◀ 1⃣Andaa maji lita 12 kisha tia humo tigna na koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando. 2⃣Chukua sless koroga ndani ya maji lita 12 hadi iyeyuke kabisa kisha weka kando. 3⃣Chukua maji nusu lita korogea humo chumvi 500gm hadi iyeyuke yote kisha weka kando.  4⃣Chukua maji robo lita  tia  rangi na korog...

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAGADI/KIGOMA/GWANJI

Jinsi ya kutengeneza Sabuni ya magadi( gwanji)ama Sabuni ya kigoma. MAHITAJI Caustic Soda kilo 3 Mafuta ya mawese lita 20 Sodium Silicate Maji lita 10 Rangi ya bluu vijiko 3 Jinsi ya kutengeneza. 1)Chukuwa coustic soda changanya na maji na uanze kukoroga kuelekea upande mmoja endelea kufanya hivyo hadi vichanganyikane vizur baada ya hapo iache kwa saa 24 2)Chukuwa kindoo kidogo na upunguze mafuta lita 3 kwa ajili ya kuweka rangi pembeni,weka rangi vijiko 3 ,changanya na mafuta uliyopunguza lita 3 kisha koroga mpaka yachanganyikane vizur kabisa 3)Chukuwa coustic soda uliyoloweka kwenye ndoo kubwa ,kisha tia mafuta na uendelee kukoroga kuekekea upande mmoja kwa nguvu na kwa haraka,tia sodium silgett kwa kunyunyuzia kidogo kidogo, endelea kukoroga hadi vichanganyikane viwe kitu kimoja 4)Baada ya hapo andaa ndoo nyingine ndogo ,chukuwa uji uliokoroga au mkorogo wako kias kwa ajili ya kuchanganya na rangi mwanzo na mafuta kisha koroga kwa pamoja vichanganyikane vizur ...