Fursa za mtaji wa laki moja (100,000) kwa wajasiriamali
wadogo
Laki moja naweza kufanyia biashara gani?
Fursa za laki ni nyingi sana kwa alieamua kutoka ndani na
kuingia mtaani. Kabla hujaendelea naomba nikupe angalizo.
Kama hujaamua kutoka ndani na kuingia mtaani ama kwa lugha
nyengine kama hujaamua kufuta aibu kichwani mwako basi hii makala haikufai.
Fursa hizo ni kama:-
MAMA NTILIE, KIJIWE CHA CHIPS, KIJIWE CHA SUPU, KIJIWE CHA
NYAMA CHOMA & MISHKAKI, KIJIWE CHA PWEZA, KIJIWE CHA MATUNDA (MATIKITI YA KUCHONGA),
ETC
Kwa kawaida kila penye watu wengi ambao huwepo kwa muda
mrefu basi pana wateja wa aina 2. Wa kipato kikubwa na kidogo.
Maeneo mengi yenye watu wengi panakuwa na migahawa kadhaa.
Mathalan kwenye mahospitali makubwa kama muhimbili, kwenye vituo vikubwa vya
mabasi kama ubungo, kwenye viwanja vikubwa kama taifa, etc.
Humu kote kuna migahawa. Unachopaswa kufanya ni kuangalia je
hisi sehemu zinapatikana milo ya kimaskini? Assume mtu ana nja na bajeti yake
ni 1000 tu je unaweza kumuuzia chakula kwa bei hiyo?
Wengi wa hawa wa bajeti za chini wanachoangalia zaidi ni
chakula kisafi cha kushiba. Hawana mbwembwe ya mboga mbili tatu. Hata kama ni
wali maharage ni sawa tu ilimradi iwe katika bajeti yake.
Makala hii itaendelea. Tutapitia fursa nyingi sana za mtaji
wa laki moja. Usikose kuendelea kufuatilia ukurasa huu.
Nini cha kufanya kama una mtaji zaidi ya laki
NINI CHA KUFANYA KWA WENYE MITAJI MIKUBWA?
Kabla ya kuendelea na zile fursa za biashara za laki moja
nimeona nitoe angalizo kwa wale wenye mitaji mikubwa kiasi.
Ukiwa na mtaji mkubwa kiasi haina maana kuwa ndio ujiingize
katik idea kubwa kubwa. Bali ingia kwenye idea ndogo ndogo na uzifanye kwa
ukubwa.
FAIDA YAKE
Faida ya huu mtindo ni kwamba unaweza kuisoma biashara na
kuiteka gafla. Mfano ni mtindo anaoutumia Bakresa kuzichukua idea ndogo na
kuzifanya kwa ukubwa.
Tumeona ice cream, tumeona juice, tumeona ukwaju, tumeona
karanga, tumeona ubuyu, na kadhalika na kadhalika.
MFANO
Labda wewe una milioni kumi ama zaidi na unawaza biashara ya
kufanya. Unaweza ukachukua idea hizi za laki ukazifanya kwa ukubwa zaidi kama
anavyofanya Bakresa.
Tuchukulie umeamua kuifanya ile ya mayai. Utakachokifanya ni
kuifanya kwa kiwango cha kisasa na kikubwa.
Wale vijana kwako watakuwa mawakala. Mtaingia mikataba.
Utawapa tisheti. Utawapa kiwango wanachotakiwa kuuza kwa siku. Utawapa mafunzo
ya ujasiriamali na utawalipa commission. Watauza kama wale wa Baressa
wanavyouza ukwaju.
Inatakiwa pia kujenga brand mitandaoni. Hakikisha unakuwa na
posts nyingi sana zinazoongelea biashara hii. Usione hasara kuwa na camera man
wako maalum kwa siku awe anapiga picha za kutosha na ku edit.
ANGALIZO
Biashara ndogo ni nyepesi wengine kuiga hivyo unatakiwa kuwa
na ubunifu wa ziada. Kila mara kaa na watu unaoamini kuwa wana ubunifu na
wakupe maoni yao.
Bahati mbaya sana watanzania tukishasimama katika biashara
tuna ignore kutafuta ushauri mpaka tuanguke.
Ukiwa karibu na wabunifu ni rahisi kutumia hili gurudumu
kupanua wigo wako kila mara kuliko kusubiri wengine waige na kuanza kulalama.
Fursa namba moja ya mtaji wa laki moja
Mradi wa kwanza wa laki moja ambao nitauzungumzia ni wa
biashara ya mayai ya kuchemsha. Mradi huu utakuhitaji kuajiri kina/binti mmoja
au zaidi kulingana na upatikanaji na uaminifu wa vijana ambao unahisi watakufaa.
Katika mfano wangu ambao nitatumia eneo la dar:
Nita ajiri vijana
watatu ambao nawafahamu mwenendo wao.
Nitanunua mayai trey
9 pamoja na trey zake. Hapa nitatumia kati ya 70,000 hadi 90,000.
Nitanunua chumvi
pakti moja.
Nitachemsha hayo mayai trey zote 9.
Kila kijana ataondoka
na trey tatu asubui na kwenda kuuza maeneo ya mchanganyiko ikiwa either ni
stendi na sehemu kama hizo.
Makubaliano kwa vijana hao watatu ni kwamba kila trey ambayo
mtu anauza nitamlipa shilingi 3000. Na bei ya yai wanapaswa wauze shilingi 500.
Mapato kwa siku ya kwanza yatakuwa 500x30x9 = 135,000. Kati
ya hizo nitawapa vijana shilingi 9,000 kila mmoja.
Ratiba itaendelea hivyo kwa muda na nitapanua biashara
itakapobidi.
Gharama zingine ndogo ndogo ni kama mkaa na chumvi na ni
kiasi kidogo sana.
Hivyo gharama zetu ni:
Mayai na trey zake = maximum 90,000
Malipo kwa vijana = 27,000
Chumvi, mkaa = 3,000
Jumla 120,000.
Mauzo 135,000 toa gharama 120,000 sawa na faida 15,000.
Kuanzia siku ya pili faida itaongezeka mana hatununui mayai na trey zake bali
tunanunua mayai pekee.
Fursa namba mbili ya mtaji wa laki
Fursa ya pili ya laki moja ambayo nitaizungumzia ni biashara
ya genge. Genge ni sehemu muhimu sana katika maisha ya mitaani. Wachache sana
huku mitaani kwetu ambao huenda shopping ya kujaza vitu ndani.
Wengi wetu hununua mahitaji ya papo kwa papo. Hebu toka
tembea tembea na uangazie mazingira ya mitaani kwenu, mitaa ya jirani, mitaa ya
mbali kidogo, mitaa ya sokoni, etc.
Katika tembea tembea yako angalia ni wapi pana uhaba wa
magenge. Na pia unapopita magengeni angalia viashiria vya soko kuwepo. Ukipita
sehemu ukaona watu husubiria kuhudumiwa mmoja mmoja na wapo wengi jua kuwa hapo
kuna fursa kubwa sana.
Pachunguze na uorodheshe mambo ambayo kwako unaona ni
mapungufu ya hilo au hayo magenge. Ukishaorodhesha mapungufu angalia na ubuni
njia ya kuwa na genge ambalo litatoa nafuu kwa wateja.
VITU VYA MSINGI GENGENI
Mboga majani
Vingia mchuzi kama
nyanya, carrots, hoho, vitunguu, etc
Viungo vya ziada kama iliki, dalasini, swaumu, etc
Matunda kama tikiti, tango, chungwa, papai, parachichi,
embe, nanasi, etc
Viazi, nazi, ndizi mbichi, etc
NJIA ZA KUJUA FAIDA
Kupata urahisi orodhesha hivi vitu katika karatasi ya
shopping na uweke idadi. Ukimaliza pita magenge kadhaa na ukifika uliza bei ya
vitu hivyo na uinakili.
Ukimaliza nenda sokoni wanapouza bidhaa hizo bei za jumla.
Uliza bei na uorodheshe bei hizo.
Fanya hesabu katika laki moja utaanza na idadi gani ya vitu
gani mana hutomudu kuweka kila kitu kwa laki moja ila pia hutokosa soko hata
kama utakuwa na vitu vya elfu 20.
Ukishamaliza hesabu za hapo juu linganisha jumla ya pesa
utayotumia ukinunua vitu hivyo kwa bei ulizoona sokoni na jumla ya mapato
utayoyapata ukiuza bidhaa hizo. Tofauti yake huwa ni faida yako.
KWA MFANO
Kwa kawaida sado moja ya viazi utauziwa kati ya 3,000 hadi
4,500 kulingana na sehemu. Tathmini kadhaa zilizofanyika zinaonesha kuwa sado
moja huingia wastani wa mafungu 9.
Kuna baadhi ya sehemu mafungu hayo wanauza kwa 500 na sehemu
nyengine wanauza kwa 1000.
Ukinunua sado moja kwa 3,000 ukauza fungu kwa 500 na
ukapanga fungu 9 utapata 4,500. Hapa faida ghafi ni 1,500.
Ukinunua kwa 4,500 ukapanga fungu 7 na kila fungu ukauza kwa
1,000 utapata 7,000. Hapa faida ghafi ni 2,500.
Kwa ufupi katika biashara ya genge katika kila 10,000
unayoingiza faida chache sana utayoipata ni 2,500.
Sasa kazi ni kwako kuangalia sehemu yenye mzunguuko mzuri.
Ukiuza bidhaa za 60,000 kwa siku utapata zaidi ya 15,000 faida kwa siku.
Itaendelea.......................................
>> Endelea
kufuatilia makala yetu kila siku.
Comments
Post a Comment