WAZO LA BIASHARA
IDEA ya Biashara ni moja ya mambo yanayo waumiza watu wengi
sana, Na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kuja na
wazo lenye tija kwako na kwa jamii nzima.
HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA
1. TUMIA UJUZI ULIO NAO
Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la
Biashara, Mfano kama wewe umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, why usianze na
wewe kuwa na biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari why usianzishe
gereji yako?
Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza nay a kipekee ya kupata
wazo na mara nyingi wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya
na kwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe
2. BADILISHA HOBBY YAKO KUWA PESA
Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, kama
wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga mbwa?
Kama Hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usinzishe mabwawa ya
kuogelea na wengine wakawa wankuja huko kuogelea?
Kama wewe hobby
yako ni upishi kwanini usianzishe mgahawa wako na ukaanza kuuza chakula?
Kam unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya
landscape gardening.
3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYARI IPO
Ukishindwa kabisa kupa wazo mwanana unaweza nunua biashara
ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa
sababu mbalimbali so unaweza nunua nu kuendelea nayo.kwamfano Maduka makubwa ya vyakula, mahoteli,
Super market n.k
4. KUNUNUA FRANCHISE
Hii ni moja ya njiza zinazo tumika kwa sasa na sehemu nyingi
sana, Unaweza nunua Popular Brand na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna
mashariti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brandi
yenyewe, nah ii ni popular sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA
MADUKA MENGINE.kwamfano
unaweza nunua brand ya kampuni ya Usafirishaji kama vile SUPERFEO na kutoa
huduma sawa na wao.
Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa
Taarifa make inaweza kula kwako na ukajikuta unafilisiwa.
5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu unakuta either ni Mrembo sana, Handsome na
kazalika, unaweza utumia huo urembo na uhendsaamu kufanya biashara, either za
marketing,mitindo n.k
6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa
opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenum au
maeneo unayo enda kustarehe.
-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia
muda mwingi na pesa nyingi?
– Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za
muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia
sana mtaani hapo?
7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za
utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.
8. TUMIA TEKNOLOJIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika
kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa
unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara.
9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI NYINGINE WANAHITAJI
NINI?
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani
maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali,
Makampuni kama Viwanda Migodi na kadhalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza
kuwa wanahitaji kwa wingi.
10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na
kuuza
11. ANGALIA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna chaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na
biashara, hata TBC huwa ina makala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za
kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali,
so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango w akutosha kwa wewe kupata wazo
la biashara
12. COPY BUSINESS IDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copy
idea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa
kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika
13. TUMIA NJIA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA BIASHARA
– Maonyesho ya biashara
– Magazeti,
– Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
– Kwa marafiki.
14. UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina
Thomas Edson Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikio kwako.
Kwa maoni
zaid toa comment yako hapo chini
Nyamka company
ltd
www.nyamkacollection21.blogspot.com
Kiukweli unatufungua ubongo xaana! Nimeudhuria semina nying za ujasiliamali lkn kwako nimepata v2 vpya kabisa
ReplyDelete🙏shukran
shukrani sana kiongozi
Delete