Mambo 5 Ya Kufanya Kwenye Mtandao Kuwafikia Watu Wengi Na
Kuuza Bidhaa Nyingi.
Kama wewe ni mjasiriamali mwenye bidhaa au huduma nzuri
lakini unashindwa kuwafikia watu wengi kwenye mtandao basi hakikisha unanipa
macho na masikio yako kwani huenda makala hii ikawa moja ya makala muhimu
utakayosoma mwaka huu.
Kutokana na uzoefu wetu wa kutumia mtandao kwa miaka zaidi
ya 6 kupata wateja, tumegundua kuna mambo 5 ukiyafanya vizuri basi utawafikia
watu wengi na kuuza bidhaa nyingi sana.
Mambo yenyewe ni:
1. Zingatia Ubora:
Zingatia ubora
Ukiwa unatoa bidhaa au huduma nzuri kwenye soko yenye
kutatua matatizo ya wateja wako, basi utapata majeshi ya watu watakaokusaidia
kusambaza ujumbe kuhusu bidhaa yako bila ya wewe kuwalipa chochote.
Wajasiriamali wa Silicon Valley, Marekani wana msemo wao
unaosema,
The goal is to develop a product so good that customers will
move the products for us before we consider marketing it.
Yaani,
Lengo ni kutengeneza bidhaa nzuri sana kiasi ambacho wateja
wetu watatutangazia kwenye soko kabla ya sisi kufikiria kuitangaza wenyewe.
Na moja kati ya sifa muhimu wawekezaji wa makumpuni ya
Silicon Valley (akina Facebook) wanaangali ni bidhaa nzuri zinazoweza
kutangazwa na watumiaji!
2. Kuwa Tofauti
Kuwa Tofauti - Jinsi Ya Kutumia Mtandao Kuwafikiwa Watu
Wengi
Ukiwa tofauti unakumbukwa.
Moja ya kosa kubwa linalofanywa na wafanyabiashara wengi ni
kuangalia washindani wako wanafanya nini na kuwaiga.
Ukifanya hivyo basi usitegemee biashara yako kudumu miaka
mingi.
Kuwa mbunifu na jiweke tofauti kabisa na washindani wako.
Mfano mzuri ni kampuni ya viatu iitwayo Vibram Five fingers,
viatu vilivyokaa kama glovu za mikono.
Vibram 5 Fingers - Viatu kama gloves
Walipoviingiza viatu vyao sokoni vilianza kuenea kama virusi
vya flu na kila aliyekuwa anaviona viatu hivyo alikuwa akivitamani.
Kwa nini? Mbali na bidhaa yao kuwa nzuri, walikuwa tofauti
kabisa na viatu vyengine.
Ukiwa tofauti utakumbukwa siku zote.
Hutafananishwa na mamia ya washindani wako wanaofanana.
Na kila ikiwa rahisi kukumbukwa inakuwa ni rahisi vile vile
kuwafikia watu wengi.
3. Toa Kabla Hujapokea
Toa kabla hujapokea - Jinsi ya kutumia mtandao kuwafikia
wateja wengi
Japokuwa umeanzisha biashara yako kutengeneza pesa, jiulize
kitu gani unaweza kutoa BURE kabla ya kuuza bidhaa yoyote?
Hii ni muhimu sana kwani wateja wako watarajiwa hawakujui,
hawakupendi na wala hawakuamini.
Kwa hivyo ukiwazawadia kitu chochote, utajenga uaminifu kwa
urahisi na kwa kasi kubwa sana hususani katika mtandao.
Vitu unavyoweza kutoa ni kama:
Ushauri
Sampuli ya bidhaa
Mafunzo (kama haya tunayookupa sisi)
N.k. (Kuwa mbunifu)
Lengo la utoaji ni kuwaonesha wateja wako watarajiwa kuwa
haupo pale kula pesa zao bali unawajali na unataka bidhaa / huduma unayotoa
iwasaidie kutatua matatizo yao.
4. Tengeneza Smaku Ya Kunasa Wateja Kwenye Mtandao
Nasa wateja kama smaku
Tengeneza mashine kwenye mtandao yenye kuwasiliana na wateja
wako watarajiwa, kukujengea uaminifu na kukuuzia bidhaa zako kwa niaba yako.
5. Tangaza! Tangaza! Tangaza!
tangaza. Jambo la tano na la muhimu sana la kufanya kuweza
kuwafikia watu na kuuza bidhaa nyingi ni kutangaza.
Matangazo ni kama petroli kwenye gari lako.
Ukiacha kutangaza biashara yako haisogei mbele. Inakwama au
inarudi nyuma.
Kwa vile washindani wamekuwa wengi kutangaza si jambo la
hiari.
Ila ni muhimu kuzingatia matunda unayopata kutokana na kila
tangazo uweze kuboresha na yazidi kukuletea faida.
Lengo ni kuwekeza pesa yenye kukusaidia kuleta mauzo yenye
faida kubwa kuliko gharama za matangazo yako na kuendelea kufanya hivyo kila
siku ili biashara yako ikuwe.
Ukiwa na mfumo mzuri kwenye biashara yako (ya mtandaoni na
nje ya mtandao) kazi yako kubwa itakuwa ni
Kutangaza na
Kuboresha bidhaa na huduma zako
Natumai umefaidika na makala hii.
Tujulishe kwa ku comment hapo chini, njia zipi unazotumia
kwenye mtandao kuwafikia wateja wako.
Comments
Post a Comment