DALALI WA NYUMBA
APP ya udalali wa nyumba, kila siku watu wana tafuta chumba
au nyumba kwa lengo la kubadilisha madhari. Dalali wa nyumba au vyumba ni kazi
sana kumpata kama unahamia sehemu ambayo wewe ni mgeni , madalali wengi ni gharama
sana kuzungusha sehemu wewe unataka. Kuna changamoto kubwa sana kwenye kutafuta
chumba au nyumba kwa kutafuta madalali na kupata chumba ambacho unataka pia ni
changamoto kubwa na inachukua muda mrefu.
APP ya udalali zipo lakini bado hazijatatua matatizo ya watu
kupata chumba kirahisi, APP bado ina kuunganisha na madalali wa kukutafutia
chumba. APP ilipo bado haimpi mtu
uwakika wa kupata chumba kwa wakati au anachokitaka.
Suluhisho la tatizo la kutafuta chumba au vyumba ni
kutengeneza APP ambayo inaongoza mpangaji na mwenye nyumba moja kwa moja na
kuchangua chumba au nyumba viliivyopo kwa mwenye nyumba husika.
Akishapata chumba/nyumba analipia kodi ya miezi 6 + kodi ya
mwezi 1 ya dalali (kamisheni) kwa kutumia tigopesa/airtel money/mpesa/halopesa
kupitia APP, na malipo yote yanatumwa kwenye akaunti ya kwenye APP paka
mpangaji kuhamia kwenye nyumba/chumba ndiyo pesa inaitumwa kwenye akaunti ya
mwenye nyumba.
Njia ya kufanya ili kufanikiwa kwenye hii Project ni kama
ifuatayo:
Sajili APP yako kama kampuni (Brela)
Ingia kwenye mfumo wa kodi TRA na kupata TIN
Sajili manispaa kwa kupata leseni ya biashara yako
Fungua banki akaunti
Fungua COLLECTION ACCOUNT kwenye kampuni ya simu (Tigo,
Vodacom, Airtel na Halotel)
Weka masharti ya kusajili kwenye APP na matangazo yao
kuonekana ni lazima wenye nyumba kuweka Hati ya nyumba, National ID, na picha.
Weka limit ya kweka picha ya nyumba au vyumba kwenye APP(min
6 pics).
Namna APP itavyokuwa inafanya kazi:
Mpangaji ana jisajili kwa kuweka namba ya simu na majina yake
mawili.
Mpangaji ana chagua vyumba au nyumba ambavyo vinapatakana
kwa sehemu husika kwa kuchagua sehemu mfano wilaya->kata->mtaa
Mpangaji akishapata chumba anachokipata analipia na peka
inaingia kwenye collection account kabla haijatumwa kwa mwenye nyumba.
Chumba kilicho lipiwa hakitaonekana paka mpangaji ahame
kwenye hiyo chumba au vyumba.
Mpangaji lazima aongeze kodi ya mwezi 1 kama kamisheni ya
dalali.
Comments
Post a Comment