BIASHARA YA STATIONARY
Biashara ya stationary imekuwa maarufu sana tanzania nzima,
wanaofanya wengi wanajua vitu ambavyo wengi wanajua ndo maana wanagawana wateja
na baadhi ya waanzilishi wanashindwa na kufunga ofisi.
Wengi wanafanya biashara hii kwa mazoea na sio kwa ubunifu
na mwendelezo wa kujifunza zaidi na zaidi na kuwa bora kwenye kazi yake.
Wengi hawajui kubuni kazi mpya zinazotokana na printing,
wengi wanatumia PUBLISHER kutengeneza kadi n.k bila kujua kuna kitu kinaitwa
ADOBE ILLUSTRATOR, ADOBE PHOTOSHOP, ADOBE FIREWORKS n.k ambazo ukitumia hizo
software unatengeneza kadi ambazo utakuwa tofauti kabsa na wengine , ila watu
wanapenda vitu virahisi ndo maana hatuon faida kwenye stationary baadae kufunga
ofisi na kutafuta biashara zingine.
Kama unataka kufanikiwa kwenye biashara ya stationary fuata
hatua zifuatazo bila kuruka:
1. Penda kujifunza zaidi kuhusu huduma zitokanazo na
printing. Usipenda rahisi kutoka publisher wengi wanafanya na kufanya wateja
wasione utofauti na kwenda stationary ile wanayoiona mbele yao.
2. Kuwa mbunifu. Buni kitu ambacho kitakitofautisha na
wengine na kuwe kwenye category mpya ambayo sokoni haipo. Google Google Google
ni dizan gani mpya ya kutengeneza kadi kwa sasa.
3. Jifunze kununua vitu online na sio tz. Fanya jitihada
yoyote kujua namna ya kununua vitu online ili uwe na sample ambazo wengine
hawana. Kuna notebook niona ebay balaa sidhan kama tz vipo.
4. Location: hii ndo kitu sehem muhimu sana kama hizo step
za juu umezifuata bila kuruka, tafuta sehemu ambayo ni karibu na chuo kikuu au
ofisi za serikali kama manispaa au tra n.k . Hizo sehemu stationary utaipenda
au kutafuta sehemu center(katikati ya mji).
5. Usipenda kufanya kazi pekeyako. Tafuta msaidizi au
mtaalamu wa ADOBE ili uwe tofauti kwenye dizani kama kadi, vipeperushi .
6. Tengeneza sample zitokanazo na printing weka sehemu
inayoonekana ili wateja waoni. Kumbuka wateja hawajui wanachokitaka paka
waoneshe, waoneshe uwezo wako kwa vitendo kuwa mtu wa kuwatamanisha vitu vizuri
ambavyo unaviona kwa wazungu na sio kwa wabongo.
7. Weka INTERNET kwenye ofisi yako. Hii itawavuta wateja
wanaoweka mavitu yao kwenye email na kutaka kuprint iwe rahisi kwao. Hakikisha
internet ipo muda wote.
8. Uza vikorokoro kama PROTECTOR, EARPHONE, COVER, FLASH.
9. Uza na movie za kudownload ili kuwavuta zaidi wateja ,
fanya mpango uwe na cumputer 2 moja ya mambo ya stationary na nyingine ya
kudownload movie , hii ya movie weka UBUNTU kuzuia virus.
10. Computer yenye UBUNTU(Windows). Hii ndio computer ambayo
mtu akija na kazi yake kwenye flash , ingiza kwanza kwenye ubuntu na kuangalia
kama ina virus ili uwatoe na kulinda computer yako ya WINDOWS 10/8/7
isihasirike na virus.
11. Nenda kwa kujiamini maofisin kuomba tenda za kuprint na
ku supply rim. Nenda ukiwa umevaa vizuri na kuonekana smart.
Usisahau kushake mkono na mkuu husika wa kitengo hicho na
kumkazia macho usoni na kusema “taja jina lako mwisho sema na furaha ya kuonana
na wewe”.
Nilijaribu hivyo nilipoenda manispaa flan mjini hapa kwenye
meeting ya kutengeneza SOFTWARE. Kumbuka “Confidence talking produce Confidence
thinking”. It work for me…
12. INSTAGRAM ACCOUNT ni lazima
“Ukitaka kufanikiwa haraka, ongeza spidi ya kufeli”
Comments
Post a Comment