BIASHARA YA SALOON YA KIUME
Biashara ya saloon ni biashara ya kawaida sana kama
utachukulia kimatazamo wa kawaida ila kama utachukulia kwa mtazamo wa kutaka
kifika mbali na kubadilisha maisha ni biashara yenye pesa sana kama utakuwa
mbunifu kwa kutumia technologia ya sasa.
Kuna msemo unasema kwamba “ukitaka kufanikiwa kwenye
biashara yoyote kwa sasa ibadilishe iwe biashara ya kutumia mitandao ya
kijamii(social media)”. Sijawai kuona mtu anatangaza biashara yake ya saloon
kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa anamini ni biashara ya kawaida sana na
haiwezi kumuingizia pesa nyingi ata akitangaza kwenye mitandao ya kijamii.
Thana potofu…
Ukitaka kufanikiwa
kwenye biashara ya saloon ya kiume fanya yafuatayo bila kuruka hatua ata moja:
- Tafuta sehemu ambayo ipo maeneo ya barabarani au yenye mkusanyiko mkubwa wa watu. Usiogope kukuta saloon zingine zipo wewe fungua kwa kuwa mbinu unayoenda kuitumia lazima wapinzani wako waombe pooo.
- Fungua akaunti ya facebook page na instagram , tangaza saloon yako ili watu waone huduma yako ili waje.
- Anzisha huduma ya malipo ya kabla, mfano kunyoa na kuoshwa ni sh 3000, madharani mtu ananyoa mara 4 kwa mwezi(4×3000 = 12000), wewe weka kunyoa mara 4 kwa mwezi ni sh 10,000; mteja ananyoa kila wiki ndani ya mwezi mzima(ndevu na nywele). Swala hili litangaze mara nyingi kwenye mitandao ya kijamii uku ukilenga mtaa ofisi ilipo( tabata segerea BIMA) ili matangazo yako yaonekana kwa watu wa mtaani kwako tu ofisi ilipo. Kwa wanataka kulipia kila anaponyoa ni sh 3000.
- Anzisha huduma ya ushirika wa kuuza huduma, mteja akileta rafiki yake anayoa nusu bei(1500). Hakikisha huduma yako ni ile ile kwa kila mteja usioneshe upendeleo wa kihuduma kwasababu pesa ni nusu bei ya kunyoa.
- Weka tv na uwe na movie mpya mpya kwenye flash ili mteja asiboreke kipindi anasubiria huduma. Hakikisha movie ni HD na sizisho tasiriwa kiswahili.
- Kuwa mtu wa stori nyingi zenye kujenga hoja kipindi unatoa huduma usinyamaze kama bubu. Penda kutumia FOCUS QUESTIONS , ku challenge mindset za wateja wako.
- Hakikisha vitaulo ni visafi muda wote na kutumia heater kuchoma machine zako mbele ya mteja. Kufanya hivyo mbele ya mteja inaonesha unajali afya yake.
- Penda kuuliza kama mtu anapenda kuchonga au laah, vinyozi wengine wameshakalilia kila mteja anachonga bila kuliza na kuonekana anafanya kazi kwa mazoea. Usifanye hivyo wateja wengi hawapendi even mm sipendi..
- Penda kushukuru mteja anapotoa pesa na kukulipa, ni haki yako lakini wewe shukuru mzee baba.
- Post video instagram na facebook post picha kila siku saa 11 jion ukiwa unanyoa saloon. Penda kuliza mswali kujua mawazo ya wateja wako instagram na facebook. Penda sana kujua mapendekezo ya wateja wako ni yapi , wapi uboreshe ili wateja wapenda sana huduma yako na kuvuta marafiki zao kuja kwako.
- Penda kutoa ofa kila wiki kwa wateja ambao hawapo kwenye malipo ya kabla, kila wiki end au mwisho wa mwezi nyoa kwa nusu bei kama kurudisha fadhila kwa wateja wako ili hudumu nao kwenye biashara yako(Wateja wanapenda marejesho yenye faida)
- Penda kuvaa mavazi yanayoonesha unajali afya yako , swali unawezaje kujali afya ya mwingine wakati wewe yako umeshindwa, kwa lugha ya kwenye ndege wanasemaga “Vaa mask ya oxygen kwanza wewe kabla ujamvalisha mwingine”.
- Kuwa msafi muda wote kwa gharama yoyote maana ndiyo sifa pekee itakayo kufanya wateja waje kwako kwa muonekano wako kila siku. Mfano unayolewaje na mtu ananuka kwapa au anajikuna muda mwingi au mmbwa zimemjaa mwili wote paka anatisa kumwangalia. Mswaki kwako uwe kipaumbele..
- Saloon iwe safi muda wote , epuka manywel kuzaga zaga ovyo kwenye floor inatia kinyaa kwa mteja kukaa na kunyolewa. Pia yale mapazia ya kufunikiwa wateja wasitapakae nywele nayo yawe mengi kidogo na masafi kila siku.
- Fikiria kuhusu generator siku za usoni , ili mteja awe na uwakika wa kupata huduma hata kama umeme ukikatika.
“The most successful businesses today (big or small) are
those that see themselves as “technology” companies, irrespective of what
business they are in!”
ushaur mzuri sana nami nataka nianishe karibuni naomben ushauri wenu zaidi
ReplyDelete