BIASHARA YA
BAGIA ZA DENGU
Biashara ya Bagia za Dengu wengi watakuwa
wanafanya lakini sidhani kama watakuwa wanafanya kibiashara zaidi na maana
kwamba wengi wanafanya kwa mazoea, ndiyo maana biashara hii wengi wanaidharau
nakuona kama haina pesa na kufikri ni biashara ya watu wenye hali ya chini.
Biashara hii ni nzuri kama utajua sehemu nzuri ya kuweka
ofisi yako yenye mkusanyiko mkubwa wa watu, mfano chuo, stand ya dalala , njia
kuu ya barabara au karibu na barabara magari mengi yanapita.
Kwa Dar naona wengi wanafanya lakini sio wabunifu kwa maana
kwamba wanauza ila hawajali afya za wateja wao, wanauza bagia hawazifuniki kwa
kuzuia vumbi na michanga kwenye badia zao, hii ni kutojua thamani ya wateja
wao.
Kutojua thamani ya wateja wao ni kujikosesha pesa ambazo
zipo , na wengi wanakosa hizo pesa kwa kutojua ni namna gani anaweza kutumia
biashara hii kubadilisha maisha yako na kukuza biashara na kuwa kubwa zaidi na
ifikie level ya mgahawa.
Ukitaka ufanikiwe kwenye biashara ya Bagia Dengu na
kubadilisha maisha yako fanya yafuatayo:
1. Tafuta sehemu ambayo kuna watu wengi na hiyo biashara
haipo, wewe kuwa wa kwanza kuanzisha hiyo sehemu. Fanya tafiti sehem kama chuo, stand la
daladala, njia kuwa ya watu au magari.
Mfano kwa Dar unaweza weka Segerea Mwisho(Stand ya Daladala) au chuo cha
Kairuki kuna wanafunzi wengi pale .
Sehemu kama Kairuki unaweza kukaanga asubuhi au jion, sana
sana jion maana wengi usiku hawapendi kuwa vitu vizito especially wanafunzi,
wanafunzi wanapenda vitu vyepesi na vya luxury wakati wa usiku.
Kaanga bagia zako na tengeneza na kachumbari ya kublenda
kwenye machine changanya na viungo kama tango, tangawizi na pilipili hoho na
pilipili mbuzi kuweka radha zaidi , pia hakikisha umebuni kitu cha zaidi kwenye
bagia zako na kuvuta umati wa watu kuja kwako; kumbuka watu wanapenda utofauti
hawapendi bidhaa wala huduma yako.
Mfano mngine Dodoma, tafuta sehemu kama chuo cha mipango
hakuna hiyo huduma na kuna wanafunzi wengi sana pale, kuna wanafunzi wa
certificates wanaingia mwezi 7 na diploma na degree wanaingia mwezi wa 10 ,
unaweza cheza na calander ya wanafunzi kuingia na kutoka ili uingize pesa
nyingi ndani ya miezi 4 ya wanafunzi kuwepo chuo.
2. Tengeneza bagia dengu zenye ukubwa wa tofauti na zilizopo
sokoni tayari, wengi tumezoa kuona bagia dengi zenye size ndogo, wewe kuna na
zenye ujazo mkubwa kidogo kuwashangaza wateja kwa kile walichokizoea sokoni.
Hakikisha dengu imesagika vizuri ili bagia zikote vizuri na
ziwe laini zisiwaumize wakati wa kutafuna, nyingi zinaumiza wakati wa kula ndo
maana wengi hawapendi kula bagia, wewe njoo na suluhisho za kutengeneza laini
na zenye radha tofauti.
Tumia muda mwingi sana kuboresha radha au anza kufanyia
mazoezi kuhusu radha kwa kupika ukiwa home, wepe majirani kwa kupokea marejesho
kuhusu bagia zako kabla ya kwenda kuzipeleka sokoni.
3. Weka bagia zako
kwenye chombo ambacho vumbi na mchanga hauwezi kuingi kirahisi , ili kuepeka
wateja wako kula mchanga kwenye bagia, hifadhi kachumbari yako sehemu ambao
haiwezi kuchacha kirahisi.
4. Jitangaze kwenye
mitandao ya kijamii kama upo maeneo yenye mkusanyiko wa watu wengi, ili iwe
rahisi kukufuata kwenye sehemu ulipo.
Fungua akaunti instagram, na post bidhaa zako mara kwa mara,
hakikisha ikifika saa 11 jion umeshapika bagia zako na kuzipost instagram. Husisahau
hili ni muhimu sana kukuza biashara yako kujikana na watu wengi instagram.
5. Usishahu vifungashio(TakeAway), weka vifunganishio
inakusaidia kujulikana kwa mapema zaidi kwasababu kwenye vifungashio vyako
unaweka namba za simu pamoja na instagram akaunti yako, husitumie whatsapp
tumia instagram sana kwasababu ndiyo kuna watu wengi watakuona kirahisi na kuku
follow wewe na baadae kuwa wateja wako wa kudumu.
6. Siku ya kwanza toa
OFA watu waonje raha yako, usiogope ndiyo mwazo wa kuvuta watu wengi waje
kwako.Au punguza bei kwa siku ya kwanza kwa kuandika kwenye bango(Kitambaa
cheupe), na hakikisha bagia zako ziko konki kweli kweli day 1 usije
ukajichanganya kwenye hilo.
7. Dumu kwenye ubora siku zote(Be consistent), hapa ndipo
patakapo kupa umaarufu wa haraka zaidi kama bidhaa yako inakuwa na ubora kila
kukisha kama jana, hapa wengi wanashindwa kudumu kwenye ubora, mfano leo
unakuta bagia nzuri kesho zina chumvi nyingi, mara michanga , mara kachumba
imeisha bagia bado, mara bagia leo zinamafuta mengi yaani ni kizungumkuti.
Wateja wanakukimbia kwasababu unafanya biasshara na watu
wasomi kama utakuwa unafanya karibu na chuo. Ni hatari kwako kama hutozingatia
ubora.
7. Usafi ni nguzo kubwa sana ukiwa unafanya biashara ya
chakula, ukiwa msafi kila mtu atapenda kula kwako, ukiwa msafi kila mtu hata
kuwa na hofu na afya zao kuhusu kula kwako, ukiwa msafi utavuta wengi kuja
kununua bagia kwako, ukiwa msafi wengi watawashawishi na wengine kuja kununua
bagia kwako, ukiwa msafi utapenda na watu wote kwasababu umejari afya zao kwa
kiasi kikubwa.
Cheza na akili ya wateja wako na jua wanapenda nini , alafu
boresha.
8. Kuwa na uso wa
furaha mara nyingi, ukiwa na uso wa huzuni wateja wengi watakukimbia kwasababu
hutakuwa hujachangamka na kuwafanya wateja wako mudi kushuka na kuhama kununua
kwako bagia. Jiufenze kuwa na furaha ili
uvute wateja wengi kuja kwako, ukiwa mchangamfu kila mteja atakupenda kuongea
na wewe, penda kujenga hoja kipindi una wahudumia wateja wako, husipende kukaa
kimya.
9. Kuwa mkweli, husiongee
kitu ambacho hukijui, kama hujui kitu sema sijui. Kuwa mkweli ni bora zaidi
kuliko kuwa mwongo, ukiwa mwongo kila mteja hataondoa imani yake kwako
akigundua kama umesema uongo na hata amini tena bidhaa yako kwakuwa wewe ni
mwongo. Naomba usiwe wewe.
10. Tafuta jina zuri
lenye herufi zisizozidi 7(magic number), kama jina la biashara yako. AKili ya
mwanadamu ni rahisi sana kukumbuka maneno yenye herufi 7 , yakizi ni kazi sana
watu kukumbuka mfano wa kampuni kama TIGO, AZAM, VODACOM, HALOTEL, AIRTEL; haya
maneno ni rahisi sana kukumbuka . Iga mfano huu wa maneno yasiozidi 7 mfano
BAGIAORG.
11. Vaa TSHIRT ukiwa kwenye ofisi yako au unapoenda sehemu
yenye mkusanyiko wa watu , ili watu waone biashara yako kirahisi na kuvuta watu
wengi kuja kwako na kuwa wateja wako wa kudumu. Hakikisha umedizani vizuri
maneno yako kwenye TSHIRT na yasomeke kirahisi sio paka mtu azogee karibu yako.
“Usikimbilie kuwa bora, kimbilia kuwa tofauti”
Comments
Post a Comment