Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2020

FURSA ZA MTAJI WA LAKI MOJA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO

Fursa za mtaji wa laki moja (100,000) kwa wajasiriamali wadogo Laki moja naweza kufanyia biashara gani? Fursa za laki ni nyingi sana kwa alieamua kutoka ndani na kuingia mtaani. Kabla hujaendelea naomba nikupe angalizo. Kama hujaamua kutoka ndani na kuingia mtaani ama kwa lugha nyengine kama hujaamua kufuta aibu kichwani mwako basi hii makala haikufai. Fursa hizo ni kama:- MAMA NTILIE, KIJIWE CHA CHIPS, KIJIWE CHA SUPU, KIJIWE CHA NYAMA CHOMA & MISHKAKI, KIJIWE CHA PWEZA, KIJIWE CHA MATUNDA (MATIKITI YA KUCHONGA), ETC Kwa kawaida kila penye watu wengi ambao huwepo kwa muda mrefu basi pana wateja wa aina 2. Wa kipato kikubwa na kidogo. Maeneo mengi yenye watu wengi panakuwa na migahawa kadhaa. Mathalan kwenye mahospitali makubwa kama muhimbili, kwenye vituo vikubwa vya mabasi kama ubungo, kwenye viwanja vikubwa kama taifa, etc. Humu kote kuna migahawa. Unachopaswa kufanya ni kuangalia je hisi sehemu zinapatikana milo ya kimaskini? Assume